Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 29 November 2010

Ilikuwaje ulivyopata mtoto wako wa kwanza?

8 comments:

Unknown said...

Nakumbuka nilikuwa kama nimechanganyikiwa kwa furaha!! Nilikuwa kazini siku hiyo na wafanyakazi wenzangu walikuwa wakinifurahia na kunipa pongezi...

Anonymous said...

I likua kama bado niko ndotoni...furaha na raha isiyo na mfano ilitawala, kwakweli Mungu na ashukuliwe sana

Simon Kitururu said...

Hivi kupata mtoto wa kwanza kuna tofauti sana na kupata mtoto wa tatu?

Yasinta Ngonyani said...

ilikuwa ni furaha ya pekee na pia ilikuwa kama nipo ndotoni kwani nikagundua kuwa sasa nimekuwa mama. Uso kwa uso na kiumbe ambacho nimekitunza miezi tisa na sasa tunakutana....

Rachel Siwa said...

Aksanteni wapendwa kwa mawazo yenu!
kaka Kitururu si tofauti sana lakini wa kwanza anatia kama kuchanganyikiwa zaidi!
Hata mimi nilivyopata nilikuwa siamini amini hivi!

Mija Shija Sayi said...

Nilikuwa nampiga picha kila wakati yaani, wee acha tu, nilikuwa namnunulia makorokoro hadi leo hii najiuliza hivi nilikuwa natumia akili kweli au?

Rachel asante kwa kutukumbusha.

Anonymous said...

Siku zote huwa najua kuwa mama yangu ananipenda, lakini siku hiyo nilijua mama yangu ananipenda kuliko nilivyokuwa nafikiria,yaani mtoto ni zawadi moja nzuri ambayo huwezi kuilinganisha hata na utajiri. I can't explain how i felt that day!Even now i still love my mtoto, ni my comforter. Glory be to GOD!

Rachel Siwa said...

haha mapenzi tu da Mija! @Anonymous vipi ulitubu kwa mama ujeuri ulioufanya?hahaah kweli raha ya dunia ni watoto!