Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 26 February 2011

Zilipendwa!!!!!!!!

Haya wapendwa vipi mitindo ya zamani  bado inamvuto?.Je wewe  unaikubali, unaweza kuirudia au itabaki kwenye kumbukumbu!!! karibuni sana  waungwana!!!!!!

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Rachel nawe! mimi nipo tayari kuirudia na kwanza tayari ipo bomba kweli hapo wamlisahau raisoni viatu vile virefu eeeh bwana we zamani kweli mitindo ilikuwa bombi sana na pia angalia hizo nywele ...

Mija Shija Sayi said...

Umecheki na hilo gari? Yaani hapo kila kitu zilipendwa.

Mimi nazipenda staili za zamani, naona pia zinaanza kurudi.

EDNA said...

Hahaaa mimi hiyo raisoni tu,Rachael nikwambie kitu kimoja kizazi cha sasa hakina ubunifu wa aina yoyote wanachofanya ni kubadilisha majina tu,mfano raisoni sikuhizi inaitwa bwanga hicho kishati cha kubana kinaitwa kibodesuti...mimi naifagilia sana mitindo ya zamani.

MissPosh said...

Old is gold Rachel naikubali na mitindo ya zamani inarudi wamependeza simple but bomba.

Simon Kitururu said...

Mitindo ya zamani bomba yani!

Rachel Siwa said...

hahaha@ da Yansinta kweli raisoni wamemsahau! mwaka wa watoto ulikupita?

@Mija mzee wangu alikuwa anagari analipenda hilo,basi akaliandika jina nitakutajia sikunyingine sasa vipi watoto shuleni wakawa wanatuita hilo jina nikuwa nakasirika sana!!

@da Edna nikweli kabisa ni majina tuu yamebadilishwa wangu!
@ da Lisa nakuunga mkono wangu!sasa wewe nakujua ni mdau wa mitindo wangu ukiitinga ututumie pic wangu!

@ka wa mimi Kitururu nategemea siku ukivaa bwanga/buga na hizo rasta utapendeza sana!

Asanteni waungwana da Yasinta wewe umesema utakuwa wa kwanza basi tunasubiri picha wangu nasi tutajimwaga hapa au wadau?

Tuendelee na wewe je?