Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 28 March 2011

Jikoni leo ni kwa Babu Ambi!!!!!!!!!!!!!!!!

Haya wapendwa jikoni kwa babu leo!!vipi wewe binafsi kikombe cha babu Ambilikile unakiamini?.
Sema na Moyo wako!!!!!!Nasi tunataka kujua mawazo yako kuhusu jikoni kwa Babu wa Loliondo!!!!!!Karibuni sana!!.

12 comments:

Mija Shija Sayi said...

Mwinjilisti wangu Rachel hii ni ngumu sana kwa watu wazima yaani wenye afya zao kutoa jibu la kuamini au la.., hii inatakiwa tuwe tunaumwa hapo ndo majibu halisi utayapata..

Anonymous said...

Imani yako ndio itakayo kuponya.....maana dawa inamashart yakutovuka pale kijijini kwenda sehemu nyingine....kwahiyo inamaana pale ndio pateule. kwahiyo watu wakinywa wanatakiwa waishi pale wakitoka tu ninaimani dawa haita fanya kazi....Mungu anisamehe kwa kuwaza hivyo....

Rachel Siwa said...

Nikweli ugonjwa ukikupata unaweza kuchanganyikiwa hata ukiambiwa mkojo ni dawa utatafuta maji mengi unywe ili upate haraka,@da Mija sisi hatuumwi lakini tunawapendwa wetu wanasumbuliwa na magonjwa je wewe unaushauri gani kwao?.

Mimi nimekuwa na maswali mengi sana na jikoni kwa babu, Sijui ni imani yangu haba au vipi!kifupi sina imani nayo.

Mchangiaji hapo juu ni kweli inaitaji Imani zaidi!kwikwikwi wewe unawashauri wagonjwa wahamie Loliondo kwani wakitoka eneo la tukio magonjwa hayata pona!!!!

hayo ni mawazo yetu nawengine tunahitaji kuyasikia!!!!!

EDNA said...

"mfa maji haachi kutapatapa"unapokuwa na tatizo upo tayari kufanya kila utakaloambiwa ni suluhisho la tatizo lako.Ni ngumu kuamini ukiwa huna shida.

chib said...

Jiko la Babu bado halijanikuna jamani, ndio ukweli huo. Nahisi ni uongo fulani tu, kwa nini Babu anasisistiza wanaokunywa kikombe chake wasiache kutumia dawa zao za hospitali?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Babu anaanza kutuchanganya kama si kujichanganya. Je mwanzo wa mwisho wa usanii ndo unakaribia? Mara dawa inatibu mara endelea kunywa dawa! Sasa tuelewe nini au ndiyo arobaina ya mwizi inakaribia? Hata hivyo ni somo kuwa si kila ving'aavyo ni dhahabu. Poleni mtakaokuwa mmeingizwa mkenge.

Simon Kitururu said...

Mimi siamini!

Na naamini Time will tell!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kama kuna mgonjwa hata mmoja tu ambaye ameponyeshwa na dawa hii basi mimi nitaiamini!

emu-three said...

Dawa za kienyeji zilikuwepo, na dawa nzuri ni ile `haimshirikishi muumba ...' kama mtu anadai `mizimu haitaki..' hapo kuna mashaka...
Dawa za miti shamba ni tiba, lakini tusiweke eti mizimu, mashetani, sijui nini...hii sasa inaitwa `shiriki'!

Rachel Siwa said...

@ kaka Chib nimekupata wangu!
@kaka NN Mhango kwikwikwi arobaini ya mwizi!na kila ving'aavyo si dhahabu wangu!.

@mwenyewe kaka [MMN]Masangu nimekupata mkubwa!!!

chib said...

Naam, naam Da S&W, karibu Loliondo kutadoda, ni suala la wakati. He he heee

Rachel Siwa said...

haahahha kweli kaka Chib kunadoda wangu!mwisho wake utakuwa mchanga wa pwani huo mimi simo!!!!!!!!Sijui tutamlaumu nani?wanywaji,Serikali au Babu???