Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 13 April 2011

Watoto naTV!!!!!!!!

Wapendwa vipi watoto  na kusogelea TV.Kumekuwa na dhana kwamba watoto hasa wa Afrika wakikaa karibu sana na TV wanaonekana/kuwaita Washamba.Hivi unafikiri kwa nini wanapenda kusogelea TV?.Ili waone vizuri au ndiyo Ushamba? Hata hapa mtoto wangu mmoja tunakosana mara nyingi kwa tabia hiyo!!!!Wewe unamaoni/mawazo gani kuhusiana na hili? Karibu sana tuelimishane.

12 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi nina maoni tafouti...watoto ni viumbe wadadisi sana. Waangaliapo TV wakati wamekaa kwenye mbali wanaona kama hawaoni sawasawa ndo hapo inakuwa sababu ya kuwa karibu ili kuona kwa ukaribu zaidi kama kwenye kitabu nk. Wanataka kuju hizo picha zinatoka wapi na mara nyingi nimewahi kuona watoto wakitaka kufungua TV au redio na kutaka kujua sauti na pia picha zipo sehemu gani. Kw hiyo huu si ushamba. Ila si vizuri sana kwa usalama wa macho.... huu ni mtazamo wangu ruksa kupinga....

Anonymous said...

HAKUNA KITU KINACHO ITWA USHAMBA MTOTO WA KIAFRIKA /KIZUNGU KUSOGELEA TV KARIBU.LAMUHIMU HAPA NI KUANGALIA MADHARA YA MTOTO AKISOGELEA TV KWA KARIBU SI NZURI.PIA KURUHUSU WATOTO KUANGALIA TV MARAKWAMARA INA ATHARI ZAKE.KITAALAM ZILE RANGI ZIBADILIKAPO KWENYE TV ZINA ATHALI KWA MTOTO KWANI KWA WAKATI HUO UBONGO WAKEKE AMA AKILI YAKE HAIKO TAYARI KUPAMBANUA KWA USASHIHI MABADILIKO HAYO YA RANGI KATIKA TV,HIVYO NIMUHIMU WAZAZI KUWA MAKINI NA JAMBO HILI KWA UJUMLA.TUSITUMIE TV KAMA NJIA YA KUMNYAMAZISHA MTOTO AU KUCHUKUA NAFASI YA KBEMBELEZEO. KAKA S

Simon Kitururu said...

Nakubaliana na waliotangulia!

Upepo Mwanana said...

Hakuna mionzi ya TV, Mimi nashauri wakae mbali kidogo

Rachel Siwa said...

Asanteni wapendwa wangu kwa ufafanuzi mzuri na wenye kufundisha!

Nikweli tujitahidi kuwaelimisha wakae mbali.

kaka S na Upepo mwanana karibuni sana nimefuhi kuwaona!

Da Yasinta na kaka Kitururu watayarishieni japo chai wapendwa wetu,mimi leo siyo zamu yangu kupika, mimi leo ni kuosha vyombo!

hivi hii kitu ya zamu iliwakuta sijui!.

tuendelee kujifunza wewe je umamawazo gani?.

chib said...

Najivuta kwangu zaidi....
Baadhi ya watoto kupenda kukaa karibu sana na TV inaweza kuwa hawataki watu wawe wanapita mbele yao na kuwakinga kuona TV.
Jambo lingine, wanaweza kuwa na matatizo ya kutokuona vizuri vitu vya mbali, ambapo wataalamu wanasema ati wana myopia au short sightedness. Kwa hiyo wakikaa karibu na TV ndio wanaona vizuri. Cha kufanya...Jaribu kumchunguza vizuri mtoto anapoangalia vitu anapendelea kukaa karibu navyo au la, pia waweza kumpa vitu vidogo sana kama punje ya mchanga na kumuambia aishike, ukiona anaikosa kosa, basi jaribu kumpeleka kwa wataalamu wa macho wamuangalie mapema. HE Jamani hapatoshi kueleza sababu zooote za watoto kukaa karibu na runinga! Weekend njema Mama S na W

Rachel Siwa said...

Asante sana kaka Chib kwa ufafanuzi wako mzuri,kutuelimisha na kutupa elimu, jinsi ya kugundua matatizo ya macho!.

EDNA said...

Jamani sidhani kama ni ushamba, nadhani ni udadisi tu wa kutaka kujua mambo.

Mija Shija Sayi said...

Miye leo sina neno, Rachel huu uchaguzi wako wa picha umepitiliza kiwango...maana mimi kabla hata sijasoma ulichoandika nikajisemea manjula, manjula, Manjula....

Ila nakubaliana na wote waliopita.

Kazi nzuri.

Rachel Siwa said...

hahahahaa @da Mija wakina Manjula wapo wengi!!

Anonymous said...

Hey! Do you use Twitteг? I'd like to follow you if that would be okay. I'm undoubtedly enjoying your blog and look
forward to nеw poѕts.
Feel free to visit my website ; buy instagram followers real

Anonymous said...

I visited multiple web pages but the audio quality for audio songs present at this web site is truly superb.


Feel free to visit my blog - hpt