Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 14 June 2011

Penye Wengi Pana Mengi!!!!!!

 Hapa kina Mama/Wanawake wapo Jikoni na Mazungumzo yao.
Hapa kina Baba/Wanaume wapo Nje na Mazungumzo yao.

Wapendwa, Wanapokutana watu wawili au watatu hapakosi neno/maneno ya kuongea.
Na katika pitapita zangu  Mswahili mimi, Kwenye  Mikusanyiko ya Wa Afrika/Waswahili wengi kama si wote,Utakuta Wanawake/Kinamama wanakaa pekeyao na Kina baba Wanakaa pekeyao,Hata kama hawakuambiwa Kina MAMA sehemu yenu hii na Kina BABA manaombwa kukaa hapa.

Wenyewe  tu mmoja baada ya mwingine utaona wanajitenga.
Jee wewe mpenzi msomaji Unamawazo gani katika hili? Ni Utii,Heshima,Kujinafasi,Malezi tuliyo lelewa Au....
Na unafikiri wakina Mama wakiwa huko zaidi wanaongelea nini?
Na kina Baba jee?.

Karibuni sana Wapendwa Tuzungumze Pamoja!!!!

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Rochel Safi sana:-) Mimi naona ni malezi tu tuliyolelewa kwa kweli. Na mara nyingi akina mama inasemekana wakiwa peke yao basi huongea mambo ya urembo urembo na wengine husema hapo ndipo huzuko ule umbea....na wenzetu akina baba nao ni bia na pia akina mama... ruksa kupinga:-)

John Mwaipopo said...

yote uliyoyaainisha/orodhesha ni chanzo cha watu (wanaume ama wanawake) kujitenga pembeni kwa minajili ya kufanya na kuzungumza yanayowahusu. Pia majukumu ya kijamii. kwa mfano, mbali na mambo mengine, wanawake watakutanishwa na jukumu lao la kijamii la kuchota maji ama kupika. wanaume pengine kuchanja kuni.

lakini kuu ninaloliona hapa ni nia ya kutaka kujitenga. binadamu tumeumbwa na hulka ya wakati fulani kuwa peke yetu. ndio maana inaanzia katika dhana ya kuwa katika kundi dogo kati ya kundi kubwa. katika migawanyiko hiyo pia tutaona wanaoongea kabila/lugha moja watajitenga kutoka kundi dogo lililojitenga kutoka kundi kubwa zaidi. nalo hili dogo litavunjika na kututokea dogo zaidi pengine la wale wanaovuta sigara tu. nyerere alitumia dhana hii kutishia nia ya wazanzibari waliokuwa wakitaka kuvunja muungano akiwaambia wakiwa peke yao (wazanzibari) watajiona miongoni mwao kuna wazanibari na wazansibara.

pamoja na faida za umoja ni nguvu (na utengano ni udhaifu), mwisho wa siku binadamu tunapenda, japo kwa masaa fulani, kuwa peke yetu. dhana inaanzia katika kundi dogo kumeguka na kuwa kundi dogo zaidi. hivyo hivyo mpaka mtu anataka kuwa pekee.

hebu jiulize je kuna wakati utatamani kwenda chooni na mtu mwingine kunanihii?

Mija Shija Sayi said...

Aisee mwaipopo umeongea yote. Hili suala la kujitenga ni muhimu sana kwa kujijenga. Binafsi huwa najitenga kila alfajiri kukiwa bado kimyaaa...

Rachel asante kwa topiki.

Simon Kitururu said...

Jamani Msinitenge! Inamaanisha navyojipendekeza kuna kitu naharibu?

Ila nasikia asili ya watu kupennda kujitenga ni walipo zalishwa . Kwa kuwa ya siri yazalishayo mpaka watoto nasikia hayafanywi hadharani!:-(

Goodman Manyanya Phiri said...

Kujitenga ni sawasawa tu na kukumbatia chombo cha ujinga.


Nauliza: Je ukiwa mwanamama mjamzito utamkataa daktari wa kiume akusaidie kuzaa kwakuwa eti yeye hana kizazi?


Wewe mwanababa utamkataa mkufunzi wakike chuoni akupe somo "HOW TO BE A GOOD FATHER" kwa kuwa yeye ni “maza” wala sio “faza”?

EDNA said...

Wakati mwingine mwanaume/mwanamke huwa comfortable kuongea au kufanya jambo fulani pale anapokuwa na watu wajinsia yake...Kwa mfano wanawake wakikutana wataongea kuhusu urembo, jinsi ya kutunza nyumba, familia na mambo mengine mengi.Sasa kama kulikuwa na mwanaume hapo akishasikia mmeanza ongelea habari za urembo lazima ataondoka..

Umenifurahisha kwa kulileta hili jambo da Rachel,Coz juzi mimi na shemeji yako tulienda mtembelea rafiki yangu, kufika pale rafiki yangu naye akawa amemkaribisha rafiki yake mwingine,kwa hiyo wanawake tukawa watatu mwanaume mmoja.Maongezi... yakaanza mwanzoni yalikuwa ni maongezi ya jumla,lakini baadae tukajikuta tumemtenga mwenzetu tumeanza kuongea ya kwetu.Heee jamaa akaona mmmh hapa hapanifai ikabidi aage na kusema wee endelea nitakufuata baade...

emu-three said...

Hilo neno kuitenga, naona ni asili, kwanii wanawake wana yao yakuongea na wanaume wana yao,na pia maumbile nakadhlika, mkichanganyikana itawia vigumu kwa wengine kukaa huru..zipo sababu nyingine za ki-imani na kiitikadi...lakini sio kujitenga kwa nia mbaya!
Swali ni je wanazungumza nini? mara nyingi asilimnia kubwa kwa wanawake ni urembo, shughuli na kusengenyana, na wanaume...mmh, kuonyeshana nani zaidi, mke aina gani ni mzuri, hata kuteta, wapo wanaume wana tabia hiyo pia....na vitu kama hivyo!
Nami nichukue nafasi hii kuonyana kuhusu `dhambi ya ulimi' kusengenyana imekuwa ni jadi...sio vizuri jamani, tuongeeni matendo na sio kuwaongelea watu...!

Rachel Siwa said...

Wapendwa wangu nawashukuru sana kwa maoni/michango, nawathamini na kuthamini maoni,Pia kuelimishana na kujifunza tusiyoyajua!Pamoja daima!!!
kama wewe ujatoa ulilonalo moyoni/maoni yako Uchelewaaaaa!!!!!

Simon Kitururu said...

Rachel asante kwako pia kwa kutuwekea kiwanja swafi!