Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 8 June 2011

Wanawake na Urembo!!!!!!!!







Haya wapendwa Urembo wakati mwingine unataka Moyo! Kama unavyoona kwenye picha.
Wewe mwanamke/dada unapenda kujiremba na unapendelea nini kuongezea Urembo wako?

Wewe baba/kaka unapenda wanawake/kina dada wanaojiremba na unapenda nini waongezee katika Urembo wao?.

Na jee kwenye Picha hizo nini kimekuvutia na nini Kimekuchukiza?.
Kwa wanaopenda kujiremba, Wanajiremba ili iweje? Ni kujiweka nadhifu,kumfurahisha mpenzi,kujipenda au.......
Na wasiopenda kujiremba, Nini sababu, Nikujiamni, kutojipenda,wapenzi wao hawapendi,kuona Aibu au.....

Karibuni sana Waungwana kwa kuelimishana.

16 comments:

Anonymous said...

Mh! huyo wa tatu NO! na huyo mwenye mikucha uchafu mtupu!

Mija Shija Sayi said...

Uzuri ni kwamba watu tunajipamba kulingana na mazingira yetu, inawezekana kabisa hao tunaoona hawajapendeza au wamezidisha maurembo labda ndio wamependeza kulinganisha na shughuli yao iliyowapelekea kujipamba hivyo.

Lakini kwa ufupi tunajipamba ili kupendeza na halafu kutoa ujumbe kwa jamii.

Baraka kwako Rachel.

Yasinta Ngonyani said...

Mimi sina la kusema kwani sipo kabisa katika fani hii. Ila nakushukuru Rachel kwa kuliweka hili wazi kwani ndio kujifunza. Pamoja daima.

emu-three said...

Sasa tunavuka mpaka wa urembo, kila jambo likizidi sana linakifu au sio, urembo wa kadri..mimi napendelea natural..urembo wa asili!

Anonymous said...

Si kwenye ulimi na kitovuni ,siku hizi ukiondoa masikio na mpaka nyeti,ni urembo au fasheni mpya ya wanadam?kazi kweli kweli

Simon Kitururu said...

Mtazamo wangu umekaa :

Kama alivyosema Da Mija kuwa mazingira tukuliayo huchangia pia tujifunzavyo urembo ndio nini!

Na kama alivyo sema Mkuu M3 kuwa ukizidisha inazidi na kupitiliza.

Ila tukumbuke mengine tudhaniayo ni urembo kwa wengine ni ishara za imani zao na wala hawafikirii wafanyacho kuwa ni urembo.

Na wengine kwenye shura hizo ni chale za MGANGA wa KIENYEJI kuzuia wachawi wasimloge mtoto na wala sio urembo . Na yale mabaka mabaka mengine ni makovu tu ya tetekuwanga.:-(


Na siunawakumbuka wale wadada Ethiopia wavaao vibakuli mdomoni?

Unaambiwa ile ilikuwa ni silaha kubwa kuliko mishale na mikuki ya wamasai kwa kuwa hakuna mMkoloni wa la makabila mengine yalikuwa yanawaingilia wale kwa kuwa ili kuwa ukitokea tu na kukutana na mdada ambaye ana tembea na bonge la bakuli kwenye mdomo wa chini hamu ya kutaka kumbaka au hata kutawala kabila hilo ilikuwa inafyata mkia.

Kwa hiyo kuna tuyaonayo kama Urembo ila shughuli zake sio lazima ni kuvutia kwa wahusika,..
... kwa kuwa zaweza kuwa ni SILAHA kishughuli au ni kiongeza starehe ndogondogo kwa wenye hereni sehemu za chini ya kitovu yale ya siri!:-(

MissPosh said...

Mhhh no wacha tupitwe

EDNA said...

Mmmmh huo urembo wa picha ya tatu unatisha jamani.

Rachel Siwa said...

Asanteni sana kwa maoni yenu wapendwa.

Da Mija lakini wewe ujatuambia unapendelea kuongeza nini kwenye Urembo wako?

@dada Lisa jee wewe unaongezea nini kwenye Urembo wako pia?@dada Edina jee nawe vipi upande wa Urembo wako hata kidogo huongezi hata kijiwanja?

Nanyie Anony je mnasemaje upande wenu?

kaka wa mimi Kitururu jee unapenda mwanamke wako/mke, Demu kristobeee aongeze nini?

@Emu-3 jee sijui nikuiteje niendelee na kaka au ok vyovyote vile unapendelea kiongezeke nini kwenye Urembo wa mwanake?

@dada Yasinta yeye kasema huko hayupoooooooo lakini dada nywele unapenda,jee unatumia nini mbona uko Mrembo ni maji na sabuni tuu?.

Kama wewe ujatoa maoni yako hujachelewa, ili tuendelee kujifunza!!!!!!!

Simon Kitururu said...

@Dada wa mimi Rachel: Mie ni mpaka nikutane na mtu ndio najua.

Nikiwa na maana nikikutana na mtu na nikastukia anabonge la chogo kama Madenge na anang'ang'ania kunyoa kipara cha wembe ndio ntamshauri kuwa labda kiurembo fuga nywele mpenzi,..
... na kama nastukia baada ya kukutana naye anabonge la kifichanyeti kama bichikoma kikupendeza wakati nafikiria thong inaweza kusaidia kuondoa bughudha fulani basi ndio ntamshauri ,..
basi mpenzi kwa kuwa si sketi ndefu,...
...labda tupunguze pichu kukubwa nifurahie sinema wakati unavua vazi mpenzi kabla hatujafanya mazoezi ya kuujaza ulimwengu kama maandiko matakatifu yatushaurivyo!:-(

Rachel Siwa said...

hahahhahhha Asante kwa maoni yako kaka wa mimi Kitururu!

Mzee wa Changamoto said...

Duh!!!
UREMBO (kama ilivyo uzuri) ni kitu ambacho hakiwezi uwa "standardized". Licha ya mazingira, kuna UTASHI. Mimi ninapotoka sijui wanatafsiri vipi urembo japo naamini kwa mwananke kuwa mrebo anastahili kuwa na (at least) 200 pounds. Hiyo inakuwa sifa ya kwanza ya UREMBO. Kisha, kulingana na "mahitaji" ya mwili, ndio unaongeza vikorombwezo.
Tatizo la ku-generalize urembo ama kujipamba ni kuwa "si viungo / spices zote hufaa mapishi". Kwa maana nyingine, wakati Mtaka-fujo Kitururu akimwambia wake afuge nywele, siamini kama ndivyo atakavyosema mpenzi wa Flaviana Matata. Lakini kama ntamwambia Mama Pau apitishe angel face, siamini kama ni urembo huu huu nitakaomwambia Koku nyumbani, ambaye ni TAFSIRI HALISI YA RANGI NYEUSI.
Kwani urembo ni nini? Na wafanya nini? Ili kiwe nini?
ALL LIES IN THE EYS OF THE BEHOLDER

Naacha
Tuonane "Next Ijayo"

Rachel Siwa said...

Hahahaa kaka Mubelwa[babake na P!]
Nanukuu;Si viungo vyote hufaa kwenye Mapishi!
Ubarikiwe kaka umepotea sana Box au.

Goodman Manyanya Phiri said...

Urembo ni sehemu moja katika taaluma mkongwe kuliko taaluma zote duniani, ile ya kupata wateja.

Hata wanaume wanajiremba tu, kwani taaluma hiyo haina jinsia! Pia nafikiri taaluma hiyo ya stahili kupewa heshima yake: wafanyakazi hao watozwe ushuru kusudi watoto wetu wasome na wajiingize katika taaluma hiyohiyo kwa hiari na sio kutokana na shida.

Naam, ninachokiona kama ni urembo mbaya, kinaweza kuwa urembo mzuri kwa mwingine!

Rachel Siwa said...

Ahsante sante sna kaka Manyanya kw maoni yako!

chib said...

Kaaaaaaaaaaaazi kweli kweeeeeeeeeli