Hapa ni mihogo iliyotiwa/kuungwa nazi ipo Jikoni .
Hapa imepakuliwa na ipo tayari kwa kuliwa.
Hii ni Mihogo iliyo chemshwa/ya kuchemshwa.
Hii ni Mihogo iliyokaangwa/yakukaangwa.
Mpendwa Leo ni Mihogo,kuna mapishi mengi katika Mihogo,wengine wanapenda Kuchemsha,Kukaanga,Kutia/Kuunga nazi.
Pia hiyo ya nazi kuna wanaochanganya na Maharage au Kunde .....n.k,Pia kuna wanaokula kwa Samaki au Mchuzi wowote.
Hiyo ya kuchemsha,kuna wanaokula kwa Kachumbari.
Kuna hii ya Kukaanga duhh hii inanikumbusha sana Shule!!Kuna wanaokula kwa Chachandu,Pilipili ya Unga,Chumvi na.....
Wewe unapenda Mihogo? Je Hupendelea ya aina gani na Kula au kuongezea na nini?.
Kinywaji gani pia unapendelea kushushia?
Karibuni sana Waungwana katika Jikoni Leo.
Nanyi pia mnaruhusiwa kutuma/kushiriki nasi, Nini unapenda au unapika.
Tuma kupitia Rasca@hotmail.co.uk.
KARIBUNI WOTE!!!!

10 comments:
mimi napenda mihogo ya kukaanga halafu ukute mihogo yenyewe ni ile enyeungaunga basi nile na kachumbari na mishikaki niteremshiee na juice
Kwanza napenda kusema nimeipenda picha yako ya prof. Kuhusu mihogo mimi huwa napenda kwanza kabisa kutafuna kama ilivyo na kutelmshia na maji...pia napenda ya kuchemsha pia kutelemshia maji au chai..bila sukari. Rachel hata mimi nimekumbuka shulenipia ..mweeehh kaaaazi kwelikweli
Mi udenda tu unanitoka!Mie kama muhogo ni mzuri vyovyote uandaliwavyo huwa napenda
nIMEKUMBUKA ...muhogo wa kuchoma nao uko juu....Pia tusisahu ugali wake:-)
futari ya 'ze hogoz' hapo juu inanivutia. mapichi mengine yanayonitia raha ni 'ze hogoz' ya kuchoma na kachumbari yenye limao. utamu wake balaa!!
Da'Yasinta ahsante sana uzalendo!
Duhhh mliokumbusha mihigo ya kuchoma yaani nimeimithi sana, ngoja siku nijaribu.
kweli kila mtu anapenda mihigo na vikorombwezo vyake, tena iwe imeiva na ungaunga kama alivyosema mchangiaji wa 1,
Tena sikuhizi hiyo mibichi inauzwa imekatwa vipande tayari kwa kutafunwa,
Eti mihogo Mibichi inasaidia majambothiiii? kaka Kitururu pole kwa udenda.
Asanteni wote kwa kuchangia na tuendelee na swali hilo la mihogo mibichi!!!!!!!!
Katika MAJAMBOTHI kuna wadaio miogo mibichi ni viagra ila mie naamini ni kisaikolojia tu!
Si unajua ukiamini chochote ni dawa na ndio maana kikombe cha babu nacho nasikia kinatibu mpaka majambothi?
Ahsante sana kaka kwajibu la mihogo na majambothi....
mwanangu muhogo wa nazi na ramadhani hii we acha tuu!!!
bampari kwa wale wa tanga school wanaijua hii lugha
Post a Comment