Bi Zaituni wa Mrisho katika Picha ndiyo Mswahili wetu wa Leo,Anaishi Ilala mtaa wa Mwanza.
Bibi huyu ana hadithi na habari nyingi sana za maisha na siasa,Leo anaongelea kuhusu ULIMBUKENI!!
Anasema watu wanaharibikiwa sana kwa kukataa yote ya zamani na kuingia kwenye mitindio mipya tuu,kwamba si yote mapya mabaya la! bali na yazamani pia yakumbukwe hasa yale mazuri, Na tuwe tunawafundisha watoto wetu,Asema utakuta mtu kazaliwa na kukulia kwenye familia ya kiswahili lakini mwaka mmoja tuu akienda nje ya nchi,anajifanya kasahau kabisa Kiswahili, mara oohh yah oohh yes, pia hawapendi hata watoto wao wanaowazaa huko au kukulia huko kuwafundisha KISWAHILI, tena na kujisifia wakipiga simu huku nyumbani mwanangu hajui/kasahau kabisa Kiswahili,Kama baba na mama Waswahili iweje mtoto wako asiongee Kiswahili?Mwisho anawatakia Waislam wote duniani Funga njema yenye baraka na amani.
Haya wapendwa Waswahili neno hilo kutoka kwa bibi unalionaje? Karibuni sana kwa kuchangia,kuelimishana na.....
Kama una lolote jema na kuelimishana , Unataka kuwaambia Waswahili wenzio karibu sana unaweza kutumia email hii Rasca@hotmail.co.uk. katika kipengele hiki cha Waswahili na Maisha yao ndani ya Swahili na Waswahili.
3 comments:
Nashukuru ndugu yangu kwa maneno hayo ya hekima toka kwa bibi na familia kwa ujumla. Ni kweli mkataa mila ni mtumwa!
BI Zaituni kamaliza!
emu-tree ndugu yangu na kaka wa mimi Kitururu bi Zetty kiboko!
Post a Comment