MELI YA LCT SPICE ISLANDERS YAZAMA KATIKA BAHARI YA HINDI PWANI YA NUNGWI LEO USIKU.
Meli
ya LCT SPICE ISLANDERS imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko
Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio
hilo limetokea saa 8:30 za usiku ambapo meli hiyo ilikuwa imebeba
abiria 610 pamoja na mizigo.
Naibu
Waziri huyo amesema meli hiyo imeondoka katika Bandari ya Malindi
Unguja ikiwa katika hali ya uzima,lakini katikati ya safari ikapata
hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.
Hadi
sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini
vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.
Naibu
Waziri Issa amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri
vya binafsi boti ziendazo kasi zimekwenda eneo la tukio kutoa msaada
unahitajika.Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helkopta yake kwenye eneo
la tukio
Awali,
amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo
baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika
kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio.
Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.
Habari kwa msaada wa Kapingaz.
1 comment:
Mwenyezi Mungu aweape nguvu wafiwa na pia azilaze Roho za marehemu mahala pema peponi Amina.
Post a Comment