Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 16 November 2011

Kuna Siku za Furaha na Siku za Vilio,Yote ni MaishaTusikate Tamaa!!!

                 Siku Ndugu zangu walipokuwa na Furaha.
                                        Mshumaa ulio Zimika.
                                            Mshumaa ulioZimika

Mungu awatie Nguvu katika wakati huu Mgumu na Sikuzote,Zaidi tudumishe Upendo,Umoja,Ushirikiano na Tusikate Tamaa,Wakati kama huu ndiyo utamjua Rafiki,Ndugu wa Kweli na Mengi Mema kwa Mabaya unaweza kuyasikia.Na niwakati kwa Waliopoteza Wazazi/Wapendwa wao Kuwakumbuka na Kulia tena,Nimeamini wanaosema Kilio hakiishi Utalia kila unapokumbuka.Nilitamani niwe nanyi lakini Mungu aliye nanyi ni Zaidi yetu sisi Tuliyo mbali.Mungu awalaze Mahali Pema Peponi Nduguzangu na Rafiki zangu,Jirani zangu na Wote waliotangulia.Sina Mengi ya Kusema bali nasema Asante Mungu.Wenu MWANAPENZA.

8 comments:

emuthree said...

Ndugu wa mimi ujumbe murua yote maisha

Phoibe Mshana said...

Ahsante sana mdogo wangu kwa salamu zako, tunashukuru sana.Mungu ni mwema siku zote, tuliwapensa wazazi wetu ila Mwenyezi Mungu amewapenda zaidi yetu. kweli ushirikiano ni jambo muhimu sana kwetu na rafiki wa kweli utamjua wakati huu!!! Ahsante sana ndugu yangu!!!

Yasinta Ngonyani said...

Rechal! Ahsante kwa kututia moyo yaani kuto kata tamaa. Pamoja daima!

Goodman Manyanya Phiri said...

Na kweli, siku haziwezi zikawa sawa... mwiko!!! (Tuthamini kivipi rangi nyeusi kama nyeupe hatujui? Na utamu uweje kama uchungu hamna?)


Labda siku moja baada ya miaka elfu hali ya binadamu itabadilika. Lakini hadi saa hiyo:


NI MACHOZI TU KOTEKOTE iwe ya huzuni au hata ya raha (na utajaza mwenyewe machozi yake Manyanya Phiri kwa sasa hivi ni yepi, kwani hata machozi ya uongo-wa-mamba YAPO TU!!!)

EDNA said...

Kamwe hatutakiwi kukata tamaa.Asante

Rachel Siwa said...

Asante sana Ndugu wamimi,pamoja sana,

Dada yangu Yasinta Pole sana ndugu yangu najua unajisikiaje mama, lakini Usikate Tamaa, Mungu ajakucha yote ni Maisha tuu dada,

Kaka yangu Manyanya maneno hayo kaka yametulia[Tuthamini kivipi rangi nyeusi kama nyeupe hatuijui?Na utamu uweje kama uchungu hamna?Ubarikiwe Msahili wa Bondeni.
Pamoja sana wapendwa!

Rachel Siwa said...

Kabisa ndugu yangu Edna mwiko kabisaa!

Rachel Siwa said...

Dada yangu Phoibe nashukuru sana, pia utafikisha salamu hizi kwa nilioshindwa kuongea nao, Pamoja ndugu zangu.