Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 17 November 2011

SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA YA JUMA PENZA[JP]!!!


Marehemu JUMA PENZA enzi za uhai wake.
Familia ya Juma Penza ya Gongo la Mboto Dar es Salaam inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana  nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa baba yetu mpendwa, aliyefariki dunia tarehe 12/10/2011 katika hospitali ya Hindu Mandal na kuzikwa tarehe 13/11/2011 katika makaburi ya Kisutu. 



Tunatoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. J.M. Kikwete, CCM Makao Makuu, ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na kwa namna mlivyoshiriki katika shughuli zote za mazishi.  Shukrani za pekee ziwaendee Dr. Macha Ocean Road, wauguzi na madaktari  wa Hindu Mandal.


Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru  kila mtu kipekee, tunaomba shukrani hizi  mzipokee  wote kwa mikono miwili  kutokana na jinsi mlivyohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha  shughuli nzima ya msiba wa baba yetu mpendwa Mzee JP.


Tunawashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu  nasi  kwa dua  na maombi wakati wote  hadi tulipompumzisha baba yetu kipenzi .


Vilevile  tunapenda  kuwakaribisha  katika  mkesha  wa dua  itakayofanyika  Ijumaa usiku  Novemba 18 kuamkia siku ya Jumamosi Novemba 19 ambapo khitma  itasomwa  nyumbani kwa marehemu  Gongo la Mboto Dar es es Salaam wote mnakaribishwa .


Tunawakaribisha wote kwenye Arobaini ya marehemu. Mkesha na kisomo utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/11/2011 na kufuatiwa na  Khitma itakayosomwa Jumamosi tarehe 19/11/2011 kuanzia saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam.Inna lilah Wainna Ilaih Rajiun

7 comments:

Anonymous said...

MWENYEZI ATUJALIE UMOJA NA UPENDO KWA WOTE,KWANI JP NDIE ALIEKUWA KIUNGANISHI CHETU CHA UMOJA WETU NA UPENDO..INSHALLAH MWENYEZI MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI...AMEEN

Rachel Siwa said...

AMINA MPENDWA,TUZIDI KUMUENZI KWA YALE YOTE MEMA ALIYOTUACHIA.

Mija Shija Sayi said...

Tuko pamoja. Amen!

Simon Kitururu said...

R.I.P Marehemu JUMA PENZA !

Rachel Siwa said...

Amina Wapendwa,Mbarikiwe sana!

chib said...

Poleni tena!

Rachel Siwa said...

Asante kaka Chib.