Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 28 November 2011

Wanawake na Urembo!!!!!!!!

                        Huyu kapaka sijui manjano.......
                        Huyu kawa wa pinki
                        Huyu na manyonyo
                                               Huyu kakaba shingo
                                                Huyu kachora .
Haya Wapendwa Wanawake na Urembo,kila siku yanazuka mapya,Pia ya Zamani yanarudi kama si kukumbukwa.Nao zamani kulikuwa na yao mengi tuu,Zazuu,Kuchoma nywele,Kusukia Rafya[sijui kama nimepatia]na Mengine Meeeeeeengi.

Wasasa kuna wanaopenda Maziwa makubwa mpaka kuyaongeza,Kujichubua/Mkorogo,Kujichora kwa sasa si hina tuu kuna Tattoo tena mpaka kwenye Nyusi, Wananyoa na kuweka tattoo ili wasipate shida ya kupaka Wanja.Kuna wanaoongeza Kope,Kunakuweka Vidubwasha ndani ya macho  na kubadili Lenzi kuwa kama ya Wadhungu. Na Mengine meeengi labda sikuweza kuyaandika au Siyajui Yote hayo kwa SABABU YA UREMBO!
Haya sasa  Mwanamke wewe;Katika hayo yote wewe unapenda nini ili uwe Mrembo au unaweza kuongezea ambayo hayapo hapo nasi Tufunguke,Pia unachukia kipi?

Wewe Mwanaume jee unapenda Mkeo,Mchumba,Rafiki yako wa Kike atoke vipi katika hayo na Unaweza kutujuza ambayo hayapo ili awe Mrembo na Unachukia kipi?

Duuhh Lakini Urembo mwingine unataka Moyo!!
Karibuni sana Wapendwa  kwa Mawazo/Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo!!!!!




10 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Urembo oyeee!!!

Juu na urembo juu!!!

Hata hivyo aina zingine za urembo si zakuigwa na wake na binti zetu.

Mtu anayenenepesha matako yake (au sehemu yake ya siri akiwa dume) huyo hana nia ya kuishi siku nyingi au kulea familia. Amejiuza katika biashara ya uasherati.


Sasa nani asiejuwa biashara hiyo imo pamoja na madawa ya kulevya, uuzaji wawatu kama watumwa, mamluki na kuangushwa kwa serikali halali za watu na maovu mengine yenye njia za haraka ya kwendea kaburini?

Yasinta Ngonyani said...

Kaaaazi kwelikweli...Mimi hapo hakuna urembo unaonifaa maana hata kupaka wanja siwezi...Halafu utakuta wengine wanaongezea kucha/kucha za bandia... kuweka karikiti ...sijui kusuka rasta/kimasai nako ni urembo? basi kama ni urembo nadhani itanibidi niache..LOL

Rachel Siwa said...

hahhah Biashara haram ni nyingi kaka yangu Manyanya!

sasa dada yangu Yasinta utaki kuwa Mrembo? tehtehteh

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! mimi naamini Mungu kaniumba urembo na kujiongezea urembo zaidi ni kujitafutia matatizo pia kumaliza pesa...Najua wengi watasema ni ubahili...na ni ruksa...

Rachel Siwa said...

Hahhahaha Nimekusoma Binti wa Ngonyani, hakika Mungu hakukosea dada Yangu!!!

Simon Kitururu said...

Ila wadada ni wazuri nyie!Wee acha tu!Tatizo tu lipo kwenye kujiamini labda!:-(

Rachel Siwa said...

Kaka Kitururu kutojiamini ndiyo kunapelea hivi ETi EEEHH,je waendelee au wasitishe?

Simon Kitururu said...

Kupendeza na kutisha labda ni mambo ya jicho lamtu tu!Na kama wajiamini umependeza jua kuna wengine watatakaoamini umependeza pia.

Upepo Mwanana said...

Huyo mkaba shingo ha ha haa

Rachel Siwa said...

Nimekupata kaka wa mimi,@ Upepo mwanana kwikwikwikwi mbona unamcheka makaba shingo, si Uzuri mwingine shurti Udhurike!!!!!