Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 14 November 2011

Wanawake Waswahili wa Coventry wanakutakia,Kila la kheri da'May!!!!!!!!

                                        Mwenyewe da'May.
                                           Kekiiiii
                                               Kata mwanangu kataaa Keki
             May akilishwa na dada yake Esther,dada huyu ndiyo chanzo cha shughuli hii
                       May akimlisha dada yake kwa Furaha
             Da'May baada ya kumlisha dada yake wakaangaliana,May akasema Asante dada yangu
                   May na Mswahili wa Congo
                Mama mwenye nyumbaaa alilishwa pia
                    dada akisogea kutoa Nasaha zake mambo ya Tanga hayo
                           Heheheheee da'Stellah Akitoa Nasaha zake
                   Weshuuu!! da'Tina akitoa Nasaha zake
                           Wamama wakifuatilia Nasaha mbalimbali
                        Waswahili kutoka Milton nao walikuwepo
                          Da'Edna alikuwa MC siku hiyo, Yupo sambamba na mwali
                           Da'Asha mwenye furaha akifuatilia mapango mzima wa Nasaha
                              Wamama hawa wameguswa na Nasaha
                          Da'Bai yupo makini na kamera yake,lakini sikio lipowazi Kusikiliza Nasaha
                     Da'Sarah,Mamie na Stellah,Shughuli ilikamalika
                                 Da'Tinna alikuwepo
                        Dadazzzz walikuwepo,Neema,Maggie na Vick
                           Penye Wanawake Waswahili hakukosi Mila babuu Mtu kwako yakheeee
                         Haya funga Vibwebwe jamaniiiii!!!!Twende sasa!!
                                Hahhahahha Mwali kakuaaaaaaaaaaa,Swahili na Waswahili Wapendwaaaa


                         Nyanyuka sasa Mdogo wangu ya Coventry yameisha Subiri ya Dar na  Tangaaa

                    Mpango mzima wa muziki na Ngoma ulisababishwa na da'Chikuuuu huyo wa Mwisho


Shughuli hii ndogo ya Kumtakia Ndoa Njema dada May,Iliandaliwa na da'Esther,yeye ni dada wa bi Arusi mtarajiwa, Wanawake Waswahili wa Coventry U.K,[WWCU]Walikuwa bega kwa bega na da'Esther kufanikisha jambo hili.
Wanawake Coventry mpo juu na Mungu awabariki sana!!!


Dada May anatarajia kufunga Ndoa hivi karibuni,Ndoa hiyo itakuwa Nyumbani Tanzania[Bongo].
Kwaniaba ya Wanawake wenzangu;Da'May Tunakutakia Safari njema,Ndoa njema yenye baraka na Mungu akutangulie kwa kila jambo wewe na Mume wako Mtarajiwa pamoja na Familia na Wote watakaofanikisha.
Mengi yalishasemwa  pale kwenye sherehe,Hatuna la zaidi sisi TUNAKUPENDA SANA!!!!!!!






5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kila la kheri na Mungu awe nanyi katika maisha ya Ndoa. Pia katika kufanikisha.

Anonymous said...

Wow nice! Wamama wakitumia chance ya kumuaga mpendwa wao, kuondoa stress zao za ndoa.

EDNA said...

Hongera mdada,nakutakia ndoa njema.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta ulikosa wewe tu, ungekuwepo ungetuonyesha Lizombe...hahahahaa!

Anonymous said...

Nakutakia kila la kheri May, umependeza sana.