Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 25 December 2011

Jikoni Leo na Xmas,Wazee wa kazi hawataki ulalamishi!!!!!!!

                                Kaka Asulwisye hapa anageuza!!
                        Hapa zamu ya kaka Hamza kugeuza.


Haya wapendwa mambo ya Xmas hayo,kaka zangu leo wameniambia,unafikiri wewe kutokuwepo watu hatuli?Wameingia wenyewe!!!!hii ndiyo hali halisi ya kwetu kwenye swala la kupika hakuna JINSIA.
Nami nawaunga mkono naona kitu si chakawaida hicho,mimi mwenyewe hapa mate yananitoka!!!


Mpendwa nawe Xmas yako imekwenda/inakwendaje? maana masaa yanatofautiana.
Wengine wameshakula na Wengine wanaandaa.


Tushirikishe basi!!!!Karibuni sana wapendwa.





5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nafurahi sana kuona kaka zetu wapo jikoni maana hii ndiyo hali niliuyokulia mimi. Na ni raha sana kuona na wengine wamo. HONGERENI SANA AKINA KAKA. kuhusu wengine Xmas ipoje mmmhhh... binafsi nabeba maboxi maakuli labda yataandaliwa jioni. BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO INAPENDA KUWATAKIA WOTE KHERI KWA NOELI KWA WOTE WATAJAOPITA HAPA.

Unknown said...

Hongera kwa kaka zetu naona mambo yao hayakwenda vibaya kabisa.. Hapa kwangu leo ni mwendo wa kikameroon tu hivyo nimejinyoosha hapa kwenye kochi nikingojea tu... Merry Xmas wewe na familia..

Rachel Siwa said...

Pole na kazi dada wa mimi Yasinta,pia nafurahi kuona malezi haya ya kina kaka si mageni kumbe,Mungu akubariki sana na familia na wapenzi wote wa RUHUIKO/MAISHA NA MAFANIKIO.

Kaka Nelson;Thank u so much and you are wellcome,I will visit your blog,May God bless u.

@Ahsante sana kaka yangu Mrope,natamani kuona hicho chakula cha Kikameroon,Uwe na wakati mwema na baraka tele.

emuthree said...

Hapa nameza mate, maana sikuu bila pilau haijakamilika!

Goodman Manyanya Phiri said...

Waache wapike wenyewe wale waalafi!!!!


(lakini tukiacha mchezo, je ni ukweli wanamama wanakula kuliko sisi wanaume?)