Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 16 January 2012

Utafiti;Eti kuangalia TV kwa saa Moja kunapunguza dakika22 za Maisha Yako!!!


  • Ukifuata kila linalosemwa na wanasayansi utashindwa kuishi. Leo watasema kunywa kahawa kunapunguza msongo wa mawazo. Kesho watasema kunywa kahawa  huko huko kunaongeza shinikizo la damu na uwezekano wa kupata pigo la kiharusi. Leo watasema hiki na kesho watasema kile ali mradi ni vurugu tupu. Kibaya zaidi ni ukimya wao kuhusu nini cha kufanya hasa pale tafiti zao zinapotoa matokeo yanayokinzana
  • Kwa vile nyingi ya tafiti hizi hufanyika huko Ulaya na Marekani, Waafrika inabidi kuyapokea matokeo ya tafiti hizi kwa uangalifu sana kwani huwa hayazingatii mazingira yetu na mtindo wetu wa maisha (japo sasa tunajitahidi sana kuwaiga kwa kila kitu).  
  • Utafiti uliofanywa mwaka jana na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Queenesland unaonyesha kwamba kuangalia runinga kwa watu wenye umri wa miaka 25 na kuendelea kuna madhara makubwa kiafya na kunapunguza muda wa kuishi. Utafiti huu unaonyesha kwamba kwa kila saa moja unayoitumia ukiangalia runinga basi unajipunguzia dakika 22 katika maisha yako. Hii ni sawa na kuvuta sigara mbili. 
  • Wanasayansi hawa wanasema kwamba tatizo hasa siyo kuangalia tv bali madhara ya kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ambako kunasababisha magonjwa ya moyo, kisukari, kunenepeana na matatizo mengine ya kiafya yanayosababishwa na mtindo wa maisha ya kubweteka (sedentary lifestyle). Kufanya mazoezi, hata kama ni dakika 15 tu kwa siku ni jambo la muhimu na kumeonyeshwa kuwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kuongeza siku tatu katika maisha yako.
              Kusoma zaidi habari hii ingia kwa  Blog ya kaka Matondo[MMN]http://www.matondo.blogspot.com
                                   Ahsante kaka Matondo.

4 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Watu wengi hawaelewi kwamba wakati unapokuwa unaangalia TV unapoteza muda wakuwa na Mungu wako. Na ndio maana Mungu anapunguza maisha kwa wale wanaopenda TV

(au niseme kwa Kiingereza)
Television has the power and does exercise it, to gear your mind into a higher level of the subconcious element which is usually found during prayerful moments. And since prayerful moments have more influential power over the ultimate outcome of your life than non-prayerful (a.k.a. "conscious mind"), the moments you spend on TV sets you as a target to the sights you witness on the box: illicit sex, graft, violence and drug abuse. So please don't be surprised to find that scientists discovered that TV watching is related to squatting on the highway to an early grave.

Yasinta Ngonyani said...

Kaazi kwelikweli, hawa wanaSayansi watatufanya tusifanye kitu sasa...

Simon Kitururu said...

Wiki ya jana niliangalia documentary mbili kwa bahati mbaya ni kwenye TV.... moja ilikuwa inaelezea jinsi bara lennye INDIA linavyoingia chini ya bara la ASIA na kusababisha kila mwaka milima ya himalaya kurefuka kitu kitakachofanya ifikie kuwa DUNIA nzima kuwa barafu kama hiyo milima ya HIMALAYA ikiwamo Everest itaendelea kukua na kubadili hali ya hewa duniani kitu ambacho kitapoza Dunia. Na baada ya hiyo nikaangalia ya Global Warming ambayo ililenga kinyume kwa kusisitizia DUNIa itazidi kuwa ya moto na mpaka sasa inazidi kuwa ya moto.

Sasa ndio hapo inapofikia umuamini nani? Na wote wanatumia vigezo vya kisayansi..

Umeniwazisha tena Da Rachel!

Rachel Siwa said...

Duhh, jamani hata mimi naogopa sana haya mambo, kila kukicha hilohilo lililo zuri leo kesho utaambiwa lina ubaya!!Ahsanteni sana kwa Maoni yenye kutufungua macho!

Kaka wa mimi Kitururu duuhh hata mimi umeniwazisha tena!!!!!