Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 13 January 2012

Wanawake na Urembo!!!!!!!!






Nimatumaini yangu woote wazima,
Haya Waungwana Wanawake na Urembo! Kuna mengi kwenye hizi picha na kwa Wanawake kwa Ujumla,
Mimi leo si msemaji saana,Kazi kwenu nyie na Mitazamo yenu,kipi wewe umependa hapo/Kukuvutia na kipi hujapenda hapo,yaani kama ingekuwa wewe hapo ungeongezea nini au ungepunguza nini,Pia wewe Mwanaume kama ni Mkeo,dada,shangazi na...Ungependa nini aongeze au  apunguze nini?Na jee labda unapenda lakini hujui ufanyeje uwe/awe kama hivyo,au kunakingine unapenda hapo hakipo,Basi usisite kusema/Kutoa Mawazo,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

Karibuni sana.


7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi kama kapulya ningependa kuwa kama hiyo picha ya juu na labda kupunguza kidogo vipodozi. Maana mimi na vipodozi hatuendi kabisa sijui kwa vile natoka Litumbandyosi? LOL

Rachel Siwa said...

Tehtehteh da'Yasinta mimi nakushauri sikunyingine jaribu walau kidogo, kwani na hilo jico dada yangu weee mama Erik tutakusahau!!!au piga mmechisho mashedoo!

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! sitaweza kwa kweli kwa sababu sitakuwa mimi tena:-) Ahsante kwa ushauri..ngoja tuone kaka zetu wanasemaje....

sam mbogo said...

Wanawake watanzania wazuri sana,niwarembo hasa!. sasa ingekuwa ndo enzi zangu, huyo wa juu kabisa anavutia, umbo lake siyo baya sana,ila vipodozi vyake havionekani vizuri. kiukweli nahusudu sana mwanamke anye kula pamba vizuri,anajipenda,huwa ni mkaguaji mzuri tu ninapo toka na wifi yenu weeeeee lazima nikubari yes sasa uko pina nayeye anajuwa lazima atakuja kuulizia mzee vipi hapa ,niko ok, basi nikumpa tu dolee, mamaaa uko safi. maswala ya ya vipodozi si mshabiki sana kuna baadhi katika picha hizi wange punguza hasa huyu wa mwisho.ila ni warembo. kaka s.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Huyo wa mwisho naona kazidisha madoido. Lakini mwingine aweza kusema pengine ndo kapendeza kweli kweli!

Swali lako halina jibu kwani hakuna vigezo vya kilimwengu kuhusu kipi ni urembo na kipi ni kibaya. Dhana ya uzuri na urembo hutofautiana katika tamaduni mbalimbali na tofauti hizi huendelea hadi katika kiwango cha mtu mmoja mmoja.

Hebu tazama post hii halafu uniambie:

http://matondo.blogspot.com/2011/02/valentine-day-mashindano-ya-urembo.html

Anonymous said...

mmh uyo wa mwisho hell no

Rachel Siwa said...

Ahsanteni sana Wapendwa kwa Michango yenu,kwani tumejifunza sana kupitia nyie,

@Kaka wa mimi Sam weweee nimefurahi sana kusikia wifi lazima akaguliwe...

@da'Yasinta hahaha hautakuwa wewe...

@kaka yangu Matondo nimepita nimekubali maneno yako kaka.

Mpendwa unayesoma hapa kama hujaisoma hiyo Post;ya kaka Matondo hapo juu,fanya usome kwani ameichambua vyema sana.

kama wewe bado unalakusema kuhusu hili mlango haujafungwa Yakheeee!!!!