Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 14 March 2012

Watoto na Urembo,Wanapaka Shedoooooo!!!!!!

Wazazi/Walezi hapo vipi?Kuna msemo sikuhizi; Aku babu najiremba mie napishana na Uzee!Nao Watoto sasa;Aku bibi nakufuata hukohuko!!Mambo ya kileo hayo, Zamani ulikuwa huruhusiwi kupaka,Wanja,Poda na vipodozi vingine, mpaka siku ya KUOLEWA!!Eti ukipaka  kabla,Siku ya Arusi hautapendeza!!Na walikuwa Wakisuka Nywele Ufunge kilemba mpaka MUMEO kwanza Aone!!''Hizi hadithi mie nazisikia''.Hahahahahha Ohiiii Leo hii nani umfungishe Kilemba?Tena ukienda salon ndiyo unafunga kilemba kama nywele zimeharibika, ukimaliza tuu kilemba kuleeee,Wataanza kuona kina baba/mama John,Juma,Neema,Pili na mnaopishana Njiani, hee dada wewe Umependeza, Umetoka Chicha na..Nani kakusuka dada mmoja anaitwa YASINTA NGONYANI!!!Muwe na Wakati Mwema Waungwa, Karibu Sana sana.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hahahahaaaaaaa...hapa leo pazuri kweli kupaka wanza katoto kama hako hadi kamenipita mie kaaaazi kwelikweli...Unajua labda mniite mshamba lakini sijawahi hata siku moja kutumia vitu kama hivyo..kusuka ndio lakini huwa nafunga kilemba na kutimka zangu kazini...mjini bila wasiwasi..na sasa nategemea kuwa naturel nimeanza kutoa rasta zangu kama kuna mtu ana muda NOMBA MSAADA KUNISAIDIA KUFUMUA maana nilisuka zile za KIMASAI:-(

Rachel Siwa said...

Hahahhahaha dada yangu Yasinta watoto wakileo hao,wanamambo haswa!Basi tengeneza Rasta za kiukweli yaani za nywele zako au vipi,Bado utakuwa kiasili zidi na utapendeza tuu.KUFUMUA NJOO HUKU TUKUFUMUE DADA YANGU!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli watoto wa kileo maana sisi wa zamani mmmhh..na nimepanga hivyo kutengeneza za asili kwa nywele zangu tu...kuja huko ungo wangu hauna mafuta...LOL

Rachel Siwa said...

Tehtehtehtehhh azima UNGO wa jilani, haahaah basi ngoja nami niangalie UNGO wangu kama umekamilika nashuka hapo si muda dada yangu!!!!!

ray njau said...

Wanawake na maendeleo songeni mbele!!!!!!!!.

Rachel Siwa said...

Asante kaka Ray!