Dr Engineer Shaban Kachua mwenye joho lenye rangi nyekundu na Bluu akiwa na waafrika wenzake wakati wa alipotunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa falsafa Nchini Canada.
Hapa Dr Kachua akiwa amekaa mstari wa mbele kabisa na wahitimu wenzake.
Mama Mzazi wa Dr Kachua (mwenye blauzi nyeusi), akiwa na Mama mkwe wake, wote kwa pamoja walishiriki katika tukio la kihistoria la kutunukiwa Shahada ya PHD kwa mtoto wao nchini Canada.
Mrs Dr Shaban Kachua (Jemima) akiwa na furaha pamoja na watoto wao walishiriki katika shughuli ya kutunukiwa Mume wake shahada ya udaktari wa Falsafa (PHD).
Kwa sasa Dr Shaban Kachua anaishi Nchini Canada pamoja na familia yake. Sisi kama watanzania wenzake tunapenda kumpongeza sana kwa kuweza kuipeperusha vema Bendera yetu, tunapenda kumshauri pia, elimu yake hiyo aweze kuitumia pia kulisaidia Taifa lake la Tanzania hasa katika nyanja hiyo ya Sayansi, kwa kutambua zaidi tuna upungufu mkubwa wa wanasayansi katika Taifa letu.
HONGERA SANA
Asanteni sana KapingaZ http://kapingaz.blogspot.co.uk/