Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 18 May 2012

MTANZANIA DR ENGINEER SHABAN KACHUA ATUNUKIWA RASMI SHAHADA YAKE YA UDAKTARI WA FALSAFA NCHINI CANADA.


Dr Engineer Shaban Kachua mwenye joho lenye rangi nyekundu na Bluu akiwa na waafrika wenzake wakati wa alipotunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa falsafa Nchini Canada.
Hapa Dr Kachua akiwa amekaa mstari wa mbele kabisa na wahitimu wenzake.
Mama Mzazi wa Dr Kachua (mwenye blauzi nyeusi), akiwa na Mama mkwe wake, wote kwa pamoja walishiriki katika tukio la kihistoria la kutunukiwa Shahada ya PHD kwa mtoto wao nchini Canada.
Mrs Dr Shaban Kachua (Jemima) akiwa na furaha pamoja na watoto wao walishiriki katika shughuli ya kutunukiwa Mume wake shahada ya udaktari wa Falsafa (PHD).

Kwa sasa Dr Shaban Kachua anaishi Nchini Canada pamoja na familia yake. Sisi kama watanzania wenzake tunapenda kumpongeza sana kwa kuweza kuipeperusha vema Bendera yetu, tunapenda kumshauri pia, elimu yake hiyo aweze kuitumia pia kulisaidia Taifa lake la Tanzania hasa katika nyanja hiyo ya Sayansi, kwa kutambua zaidi tuna upungufu mkubwa wa wanasayansi katika Taifa letu.

HONGERA SANA
Asanteni sana KapingaZ http://kapingaz.blogspot.co.uk/

5 comments:

Mtani said...

Hongereni sana mliomeremeta ... tunawasubiri mje mtusaidie kupunguza matatizo yanayohitaji taaluma zenu.

Kachiki Muke ya Mubena mimi nina-book nafasi kabisa hapa kwenye blog yako, mwaka 2025 lazima na mimi niitwe Dr. Mutani ya Kachiki.

Siku hiyo Kachiki inabidi uandaage miguu ya kuduwa (sijui itakuwa bado ina ngufu za kutoa kishindo?) na utengenesage kale kanyama special ka kule kwetu na sile mboga sa majani ambaso wengine wanasemaga ni madawa ya nanihii ... naogopa kutaja, Afande Mwema anaweza kunizukia kwenye screen, maana Mzee Makweta aliyekuwa anazipigia debe alishastaafu sijui nani atanitetea.

Once again congratulations to Dr. KACHUA and his FAMILY!

Mija Shija Sayi said...

@ Mtani, je wewe na BAP Born Again Pagan mna undugu? Yaani mmefanana sana utundu wenu...LOL!!

Hongereni sana Dr Kachua, Rachel tukaze buti na sisi tufike huko siku moja au?..

Rachel Siwa said...

Mtani;kwanza nakutakia mema sana katika safari hiyo kuwa DR.Yaani Mtani ya Kachiki wewe si wakutuma email yaani inabidi nami niwepo hapo kushuhudia ndugu yangu,Hakika utafikia tuu na Mungu yu pamoja Mtani ya Kachiki.

Hahahahha kale kanyama hatakakosa kabisa na mboga sooootee sa kwetu beehh!!.

Da'Mija yaani tena!!hayo ndiyo maneno Nasi tutafika, Tukaze kamba za VIATU DADA YANGU.

Mija Shija Sayi said...

Muke ya Dr Kachua anaonekana ana nguvu huyooo..!! Ngoja nami nianze kwenda gym...

Rachel Siwa said...

Nami nipo nyuma yako dadake!!!