Ngoma Africa band yatoa salam za hongera kwa wanahabari
Bendi ya maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU
yenye maskani yake nchini Ujerumani ,inatoa salam za hongera na pongezi nyingi
kwa wanahabari na vyombo vya habari vyote duniani,katika sherehe ya siku ya
"uhuru wa vyombo vya habari" 3 Mai 2012,bendi hiyo inawapongeza wanahabari
na vyombo vyao,kwa kazi muhimu wanazofanya za kuwapasha habari walimwengu,
kwani mchango wa wanahabari katika kila jamii duniani,ni sawa na mbolea katka maisha
ya kila siku,kwani maisha bila ya habari ,ni sawa miti bila mizizi,
Hongereni sana wanahabari na Wanalibeneke wote duniani.
FFU wa Ngoma Africa band sasa wanatamba song lao jipya
"Uhuru wa habari" wimbo ambao unasikika at www.ngoma-africa.com
au http://www.ngoma-Africa.com
1 comment:
Ndugu wa mimi lete mambo, tupo pamoja,naserebeuka na hiyo ngoma...duuuh,kumbe wamo!
Post a Comment