Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 2 June 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Tupo Burundi;Ndugu zangu wa Buyenzi Mpo?!!!!!

 Bibi na Bwana Billy.Hongereni sana Kwa kupata mtoto wa kiume.Mungu amlinde na kumkuza vyema.Nanyi awape hekima katika malezi yenu.Ngoja leo niwasogeze nyumbani.
 

Waungwana "CHAGUO LA MSWAHLI LEO" Nimewapeleka BURUNDI.
Haya umeona waRundi waishio CANADA wanavyofunza watoto wao Utamaduni wao?Jee wewe unaonaje kuhusu hili la kuwafundisha watoto mambo yakwenu?

Jee unao wakati wa kuwafundisha watoto hata Kibuzi,Kinyunyu,Ukuti,Rede,Nyimbo hata zile za Mchakamchaka?Au Muda hautoshi?

Nakumbuka kama wikimbili 2 tulikutana Waswahili kwenye Mnuso Mmoja hivi, Baada ya Kushiba Tukaanza kuimba hii Nyimbo.

Alisemaaa  Alisemaaa,Alisema Nyerere Alisema,Vijana wangu wote Mmeleegea, Sharti Tuanze Mchaka Mchaka.................Hahahahaa

 Swahili na Waswahili Waungwana.

 Kama unalolote utahitaji kuwajuza wenzio. Tutumie Kupitia Email.rasca@hotmail.co.uk.Pamoja sana!!!!!!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Rachel/kaxhiki umenipeleka mbali kweli na hapo ndo nimepapenda zaidi. Nyimbo za mchaka mchaka...Hivi hii ni nyimbo ya mchakamchaka au Askari eee vitani eeeh wanababeba bunduki bisi kibuyu cha maji....

Rachel Siwa said...

Hahaahha da'Kadala nyimbo nyingi niza Askari wazitumia, nasi tunaiga nyimbo hizo Shule kwani nasi tulikuwa Askari, tulihitajika tuwe wakakamavu. Naujua huo wimboooooooo haha Aska eee Vitani eeh.... kweli wewe Mzalendo!!!!!!!