Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 26 June 2012

DORIS KASAKA (KAPINGA) AMEREMETA KWENYE KITCHEN PARTY YAKE ILIYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA TBS - UBUNGO !!!!!!


Doris akiwa katika pozi mwanana huku akiwaangalia wageni waalikwa waliokuja kumpongeza katika KITCHEN PARTY yake 
Doris akiwa mbele ya wageni waalikwa ukumbini kabla ya kuanza sherehe yake ya KITCHEN PARTY yake .

Mama Mkubwa wa Doris, Angelina Mwami (Kapinga) akiwakaribisha wageni waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao kwenye sherehe ya KITCHEN PARTY ya Binti yake mpendwa.

Mama Mkubwa wa Doris kwa upande wa Baba, Mama Njelu Kasaka naye hakuwa nyuma kumpongeza binti yake na kuwakaribisha wageni waalikwa wote waliokuja kwenye sherehe ya KITCHEN PARTY.
Mama Mchungaji naye alifungua sherehe ya KITCHEN PARTY ya Doris kwa Sala nzuri na kukemea mapepo yote yenye nia mbaya "YASHINDWE NA YALEGEE"
KEKI YA AINA YAKE ILIYOANDALIWA KIUSTADI NA UTAALAM ALIYOANDALIWA DORIS.

Doris akikata Keki yake ya KITCHEN PARTY ikiwa ni ishara ya upendo kwa wageni wote walioshiriki katika sherehe hiyo na kula nao pamoja


Swahili NA Waswahili tunakutakia kila lililojema,Tunasubiri mnuso wa kuagwa na Ndoa.

3 comments:

wifi ya wewe.raifah mom said...

hongera sana dada doris mungu akusaidie umalizie hatua inayofuata.ulipendezaje

EDNA said...

Hongera sana mdada,karibu kwenye chama kubwa hahahaaa.Yaani hii kitchen party imenikumbusha ya kwangu kuanzia rangi,mapambo na hiyo keki duuuh au mpambaji ni mmoja?

emuthree said...

Mambo hayo, mimi thithemi kitu!