ELCT/KARAGWE DIOCESE
Kwa wadau wote wa Maendeleo
Mkoa wa Kagera
Yah: MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE
- NYAKAHANGA DDH
Somo hapo juu linahusika.
Hospitali tajwa inaadhimisha miaka 100 tangu kuanza kutoa huduma za tiba na afya katika wilaya ya Karagwe. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni: Shabaha Yetu ni Huduma Bora za Afya na Tiba
Maadhimisho hayo yatafanyika tangu tarehe 27 Agosti na kilele kuwa tarehe 2 Septemba. Katika wiki hii, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutakuwa na maonyesho yatakayoenda sambamba na utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi watakotembelea mabanda yaliyoandaliwa.
Uchunguzi wa afya kama vile Kisukari, moyo, shinikizo la damu, upimaji wa VVU, uchunguzi wa saratani ya matiti kwa akina mama, huduma za macho na uzazi n.k zitatolewa kwa kushirikiana na wataalam wa ndani na nje ya nchi.
Mbali na huduma hizo, malengo makubwa ya hospitali katika kuadhimisha miaka 100, ni kupambana na changamoto zilizopo wilayani na nchini kwa ujumla katika kutoa huduma bora za afya.
Baadhi ya changamoto hizo ni upungufu wa wataala wa kada mbalimbali na uchakavu wa miundo mbinu.
Kupitia sherehe hizi, hospitali ina mpango wa kuanzisha chuo cha taaluma za afya na tiba wilayani Karagwe mapema mwakani.
Chuo hicho kitatoa wataalam katika fani za Uuuguzi, Uganga, wataalam wa Maabara na Maafisa afya.
Ш Faida za Chuo hiki:
o Kusaidia kupunguza upungufu wa wataalam Mkoani Kagera na nchini kwa ujumla.
o Kusaidia vijana wanaomaliza elimu ya sekondari kupata elimu ya taaluma kwa gharama nafuu, zingatia mkoa hauna chuo cha waganga, ni gharama kubwa kwa wazazi kupeleka watoto wao nje ya mkoa kusomea taaluma hio.
o Chuo kitatoa nafasi nzuri kwa watumishi waliopo kazini kuweza kujiendeleza wakingali katika mazingira ya familia zao hivo kupunguza gharama na usumbufu wa kusomea nje.
o Chuo kitasaidia kuongeza ajira hivo kusaidia katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, familia na taifa kwa ujumla.
Katika kufanikisha malengo hayo, jumla ya shilingi 1.8 billion zinahitajika. Ikiwa ni kwa ajili ya uendeshaji wa maadhimisho (utoaji wa huduma bure kwa wiki ya maadhimisho), ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa chuo.
Kwa niaba ya menejiment ya hospitali, nakuomba ewe mpenda maendeleo uchangie kufanikisha malengo haya kwa maendeleo ya sekta ya afya.
Wote watakao changia wataorodheshwa katika kitabu maalum cha kumbukumbu.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu kwa Mganga Mkuu: 0762 751 335 / 0712 916 800 / 0787 785 969
Shukrani
Dr. Andrew Cesari
Mganga Mkuu
Nyakahanga Hospital
No comments:
Post a Comment