Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 4 July 2012

Wanawake na Urembo-Kunyoa Nyusi -Burudani Kipepeo!!!!!!



Waungwana Leo tuangalie Unyoaji Nyusi, Sikuhizi hata Waume wananyoa Nyusi.
Jee wewe  Unapenda kunyoa nyusi?
 Ungependa Mkeo/Mumeo,Mpenzi wako Anyoe Nyusi?


Jee unatumia njia gani?Jee unapenda kutoa zote au unapunguza tuu?


Hivi Watu wa Zamani nao walinyoa Nyusi?
Kunyoa Nyusi kunaweza kusababisha madhara yoyote kiafya?


Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.


"Swahili NA Waswahili" Pamoja sana!!!

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Uwiiiii! mama weeee ukitaka tufukuzani basi niambia hiyo kazi. sijawahi kufanya na kamwe sitafanya ngóoooooo!! Twendeni tukawinde vipepeo aiya mama vipepeo vipepeo... wimbo huo wa kipepeo umenikumbusha mbali sana ...

Rachel Siwa said...

Hahahhahah da'Kadala nahisi kama umeandika kwa sauti!!!!!

Jaribu bwana siku moja!!!jee shem yeye ananyoa?

Wimbo huo na mwenzake mabata madogodogo yanaogeleaaaaaa

Yasinta Ngonyani said...

weweeeee kachiki! acha kabisa fujo sitajaribu amini..shem? hahaaaaaa yaani nimechka kwa sauti hapa mpaka... kumbe na wewe unakumbuka nyimbo nyingiii aisee safi sana:-)

Rachel Siwa said...

Hahahahahaha OIIIIIII Yaani hapa watu wananishangaa kwa kicheko!!!!

sasa shem naye unamkataza?'Kadala utapendeza dada yangu!!

emu-three said...

Kunyoa nyusi, halafu vumbi likija machoni utalizuiaje, aua utaishia kuvaa miwani...kweli urembo upo wa dizine mabli mbali maana nsikia siku hizi kuna urembo wa uchi...unaufahamu huo, mtu anachorwa mwilimzima kama vile kavaa nguo, ...huwezi kugundua, wewe waona kavaa, kumbe duuh...

Rachel Siwa said...

Hahahaha ndugu wa mimi urembo wa Uchi...kwamwaume na Maumbile yale duuhh sijui watabandika na gundi kwani mambo si yataning'inia?

Ndugu wa mimi vumbi kwenye nyusi sasa si juu? kope ndiyo kifukuza vumbi au?
Mtaalam wa Macho kaka Chib angetusaidia hapa.

Lakini kwa nini Usijaribu ndugu wa mimi tehthethetehtehhh

chib said...

Kinachozuia Vumbi isingie kwenye macho ni kope.
Nyusi zinazuia jasho lisitiririke moja kwa moja kwenda kwenye jicho, maana jasho lina chumvichumvi ambayo huwasha jicho!

emuthree said...

Chib katusaidia ndugu wa mimi, mimi nafikiri urembo mwingine tuangalie na athari zake,...mbona miminaonanyusi ziaongeza urembokuliko ukiziondoa,sijui labda ni mtizamo wangu....ndugu wa mimi nikinyoa nyusi siku hiyo, nitaandikwa kwenye gazeti..lol

Mija Shija Sayi said...

Msema kweli mpenzi wa Mungu, mimi nadhani niko tayari kwenda...

Rachel mwenzangu vipi wewe?

Yasinta wajameni una misimamo weye...!! Ngoja nikija kukutembelea nitakushika mkono kwa mkono twende..

Chib, asante kwa somo yaani huwezi amini nilikuwa sijui kazi ya kope kama ni kuzuia jasho lisiingie machoni..

M3..upo kaka yangu?

Muwe na wakati mzuri ndugu zanguni.

Rachel Siwa said...

Asante sana kaka CHIB kuhusu nyusi kuzuia jasho nami sikujua kabisa, hakika kila kitu mwilini kina kazi yake!!!!

@ndugu wa mimi emu-3 hahaaaha!!!!!

@Dadake Mijja, Mimi nanyoa tena pale sokini bei chee kabisa!!!

Umeona eeh dada Mkuu Kadala anamisimamo yake sana, lakini ni vyema kama hujisiikii yanini uhangaike?

hahahaahha nasubiri hiyo picha da'Mija ukimkokota da Yasinta kunyoa Nyusi!!!!!