Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 25 November 2012

TAARIFA RASMI YA MSIBA WA MTOTO MARY SHABANI KACHUA KUTOKA CANADA.


Marehemu Mary Shabani Kachua (3 Yrs) enzi za uhai wake.
Familia ya Dr Shabani Kachua kutoka Canada inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Mary Kachua kilichotokea tarehe 19/11/2012 nchini Canada.
Mwili wake uliagwa jana York Funeral Home, Fredericton, NB. Canada na leo kutakuwa na misa maalum Symthe Cathedral Church, Fredericton, NB, Canada.
Familia ya Dr S. Kachua wataondoka leo Canada kuelekea Jijini Dar es salaam Tanzania kwa ajili ya kuupokea mwili na wanatarajiwa kufika kesho jumapili saa 7:30 Mchana kwa ndege ya Ethiopia Airlines.
Mwili wa marehemu Mary Kachua unatarajiwa kufika siku ya Jumatano tarehe 28/11/2012 kwa ndege ya KLM. Shughuli na taratibu za mazishi zinatarajiwa kufanyika nyumbani Tanga mjini.
Kwa mawasiliano zaidi ya taratibu zote za mazishi unaweza ukapiga namba:
+255 784 670866
+255 713 254553
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.
Amen

No comments: