Namshukuru sana MUNGU kwa yote katika mwaka huu,Yeye ni kila kitu Maishani mwangu..... Neno;Zaburi:111;1-10;Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima,Wote wafanyao hayo wana akili njema,Sifa zake zakaa milele!!!!. Nawashukuru Familia Yangu,Ndugu,Jamaa,Marafiki,Ma-blogger,Wapenzi/Wasomaji/Wafuatiliaji[Wapendwa/Waungwana]wa Swahili NA Waswahili na Mitindo Afrika .Wote wanaonifahamu kwa Namna moja au Nyingine. Nikutake Radhi/kukuomba Msamaha wewe niliyekukosea/kukukwaza kwa namna yoyote ile,Haikuwa kusudi langu kusababisha hayo ni Hali ya Kibinadamu tuu.Nami nichukue anafasi hiiKusamehe/ kusahau Makwazo, Mapito yote ni Changamoto za kimaisha na Tuanze Upya .MUNGU azidi kukubariki wewe unayesoma hapa na Wengine woteee!!!! "Swahili NA Waswahili"MUNGU atubariki Sote na Pamoja Daima. |
Monday, 31 December 2012
Shukrani Zangu na Nawatakia mwisho wa Mwaka,Uwe Mwema na Mwanzo Mzuri kwa Mwaka Ujao;Burudani-Sarah K - Niinue (Mbele Ninaendelea)na Nyingine Nyingi!!!!!!
Friday, 28 December 2012
Jikoni Leo,Afya na Jamii; Na Kaka John Haule-Jinsi ya kutengeneza maziwa ya soya.
Jinsi ya kutengeneza maziwa
ya soya.
Baba
karudi ni makala fupi fupi ambazo zitakuwa zinatoa mwanga kwa jamii kujifanyia
mambo yahusuyo afya na maisha bora kwa ujumla wa ustawi wa jamii ya watanzania
kila wiki katika uwanja huu. Lakini la kufurahisha zaidi ni kuwa, hata kama
unakusudia kufanya kitu Fulani lakini hujui namna ya kufanya basi kutakuwa na
fursa kwako msomaji kutuletea maswali ambayo naahidi yatajibiwa yote ili
kuharakisha maendeleo ya Taifa letu. Uwanja huu utaitwa “Baba Karudi” ukiwa na maana nitakuwa natoa kile nilichopata katika safari zangu
duniani kote ambako shughuli yangu kubwa ni kukutana na wataalamu wa mambo
mbali mbali na kufanya mahojiano nao halafu nakuja kuwaletea watanzania wangu
hapa vile vile nitakuwa nayapeleka maswali yenu wasomaji juu ya yale mnayotaka
kuyafanya lakini hamjui yanafanywaje.. Nakuomba usiende mbali.
Leo
nimekutana na Bi Carole Bruzzano toka www.eHow.com. Nimefunga safari kuja Canada kupata ukweli juu ya
Soya kuwa maziwa safi na bora kwa afya za walaji. Yeye anasema:
Soya
inatumika duniani kote katika mapishi mengi mbalimbali ikiwemo kutengeneza
maziwa na kuungia kitoweo kama nyama na samaki au kama mbadala wa vitoweo hivyo
kiafya kwa mlaji.
Anasema
kutengeneza maziwa ya unga ya soya ni kazi ndogo sana ambayo inaweza
kukugharimu kama dakika 60 tu. Wenye viwanda vikubwa hupitia hatua nyingi
kutengeneza maziwa hayo ya unga ya soya. Lakini wewe unaweza tu ukatengeneza
mwenyewe nyumbani kwako tena kwa kutumia vifaa rahisi vinavyopatikana bila
kuazima kwa jirani.
Wewe unatakiwa
uanze na kuzisafisha soya kwanza, halafu weka juani zinyauke kidogo ili ngozi
ya soya ilegee na kasha umenye ngozi zote, uoshe tena na uzikaushe mpaka
zikauke kau! Hapo tayari utakuwa umeshaandaa soya kusagwa na kuwa maziwa ya
unga tayari kupeleka mahotelini na majumbani kwa matumizi.
Bi
Carole anasema unahitaji kuwa na vifaa hivi:
1.
Lazima
uwe na kikaango ili uzikaange soya zako kabla ya kusagwa.
2.
Unatakiwa
pia uwe na blenda au kinu cha kutwangia na chekecheke ili soya iwe unga laini
sana
3.
Mwisho
tayarisha vikombe viwili au vitatu vya soya
4.
Maziwa
halisi japo nusu kikombe kwa ladha na harufu.
Kaanga
soya yako katika kikaango angalia zisiungue.zikaange kwa dakika 10 hadi 15 na
utaona kuwa zimeiva kwa kubadilika rangi na kuwa kahawia basi ipua na ziache zipoe
kidogo kabla ya kuanza kuzisaga.
Saga
soya zako, chekecha mpaka upate unga laini sana, ukimaliza weka katika chombo
kikavu na kisafi. Sasa chukua maziwa HALISI nusu kikombe na tia katika soya
halafu changanya na anika mpaka mchangavyiko huo umekauka.
Mwisho
utaona unga umekauka lakini bado una madonge. Yapukuchue kwa mikono safi halafu tia soya katika mkebe safi tayari kwa
matumizi kama maziwa halisi.
Faida za
Maziwa ya soya
Unaweza
kuanzisha biashara ya kuuza maziwa kama wewe ni mama ntilie au una hoteli au
aina zingine za biashara ya vyakula na ukapata faida kubwa bila kuwa na
wasiwasi wa kupata hasara.
Maziwa
ya soya ni mazuri ukilinganisha nay a wanyama kwa kuwa hayana sukari asilia
iitwayo Lacoste ambayo sio nzuri kwa afya hivyo wenye aleji na maziwa ya
kawaida basi ndio muda wao wa kujidai na maziwa haya.
Maziwa
ya soya yana protini karibu sawa kabisa na ya wanyama lakini haya yana protini
ya mimea tofauti na ile ya wanyama ambayo si nzuri kwa afya. Protini ya mimea
ni nzuri mwilini kwa kuzuia upotevu wa calsiam kwenye mkojo na kukusaidia
usipatwe na magonjwa ya maumivu ya mifupa. Wenye kisukari ndio maziwa yao
haswa.
Maziwa
ya soya hayana mafuta yenye sumu (saturated fats) wala lehemu. Hivyo ni maziwa
yanayowafaa wagonjwa wenye maradhi ya moyo sana.
Maziwa
haya bado Bi Carole anadai kuwa ni kinyonya sumu mwilini kijulikanacho kama
“isoflavones” ambacho huzuia uzee wa kizembe, maraghi ya mifupa na kansa za
aina nyingi mwilini.
Mtu
akinywa kikombe kimoja cha maziwa ya soya basi ajue kuwa ana 20%ya isoflvones
ambayo katika maziwa ya wanyama hamna!
Hivyo
leo tunaishia hapa kwa kuwaasa kujitengenezea maziwa ya soya badala ya kuharibu
pesa ambayo ni ngumu sana hasa kwa kipindi hiki. Lakini pia tumefungua rasmi
ukurasa ambao tutautumia wasomaji kuuliza namna ya kufanya jambo lolote
ulitakalo. Wiki ijayo nitakuja na “JINSI YA KUJITENGENEZEA SODA YOYOTE” au kwa
lugha ya wataalamu ni “how to carbonated drinks” ambayo itatusaidia kupunguza
manunuzi ya soda kipindi hiki cha jua kali na pia tutaongelea faida na hasara
za kunywa soda pia.
Asanteni
kwa kunisoma na tuonane juma lijalo.
John Haule ni mpelelezi binafsi
(Private investigator) anayejihusisha na tafiti zenye suluhisho kwa matatizo ya
kijamii. Unaweza kumpigia kwa miadi ya
ushauri juu ya tatizo lolote linalokusumbua kibinadamu. Anapatikana Car
Painters - Temeke Stereo, Sandawe
Street, jirani na Dr. Massawe. Simu: 0768 215 956 au email rumoursafrica@gmail.com
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Wednesday, 26 December 2012
Mfululizo wa Mahojiano ya Wadau wa Filamu na Muziki;147 Critics:John F Kitime (2)!!!
Muendelezo wa 147 Critics ambapo leo tunamsikiliza mdau muhimu na makini kwenye Muziki wa Dansi na kwa upande mwingine kwenye Filamu akielezea kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147 yanayogusa Muziki na Filamu.
Tusikilize 147 Critics:John F Kitime (2) akiwa ni mtu wa pili kuelezea maoni yake.
Msikilize vyema John F Kitime uweze kufahamu vyema yale anayoyajuwa na anayodhani ni muhimu kuwa sawa katika mabadiliko ya sheria hii!Mahojiano haya na Ndg John F Kitime yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa
nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na
hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of
artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na
vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka
stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe
rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili
kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikalimapato.
kwa Maelezo zaidi ingia;TheImageProfession
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Monday, 24 December 2012
Jikoni Leo;Tupike Pamoja-Recipe of Chicken Wings with Homemade Barbecue sauce - Mapishi ya (In Sw...!!!!!!
This is a video showing how to cook Chicken wings with Homemade Barbecue sauce, for East-African users and all the swahili speakers all around the world. It's also subtituled in English. Please, subscribe to our channel if you like it. We are working to offer you more video-recipes in swahili, in our Youtube channel and in our web-site www.tupikepamoja.com
Mmmmhhhhh Tamu Saaaana.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaaana
Sunday, 23 December 2012
Nawatakia J'Pili Njema na Maandalizi Mema ya Christmas na Mwaka Mpya;Burudani-Upendo Group Kijitonyama - Hallelujah Tunaimba na Nyingine Nyingi!!!!!!
Wapendwa;Nawatakia J'Pili Njema,Upendo,Baraka,Amani na Maandalizi Mema ya Christmas na Mwaka Mpya.
Ndugu zangu nawasihi,Waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza;Mkajiepushe nao.
Neno La LeoWarumi:16:17-20 Naye Mchungaji wa Amani atamseta Shetani chini ya Miguu yenu.Neema ya BWANA wetu YESU Kristo na iwe Pamoja nanyi.[AMINA].
"Swahili NA Waswahi" Mbarikiwe Sana.
Saturday, 22 December 2012
Mahojiano ya Wadau wa Filamu na Muziki;147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1)
Mfululizo wa 147 Critics ambayo ni mahojiano ya wadau wa Filamu na Muziki yaliyofanywa na TFCA-
Tanzania Film Critics Association(On line Platform) kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147
ambayo yatapelekea kuanzia mwezi wa January 2013 bidhaa zote za Filamu na Muziki zilizopo hapa Tanzania kuwekewa
Stamp/Sticker kwa ajili ya Kurasimisha,Kumpatia kipato halali msanii na Kukusanya mapato ya serikali yanayotokana na
uuzaji wa kazi husika.
Sheria hii ina changamoto nyingi ambazo kama hazitatatuliwa zinaweza kuifanya sheria husiaka isfikie malengo yake,Je
wadau wanasemaje kuhusiana na hilo?
Tusikilize 147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1) akiwa ni mtu wa kwanza kutupa maoni yake kupitia Video hii;
Mahojiano haya yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
98. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
ii. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kilio cha muda
mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za sanaa na
kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya. Ili kutatua tatizo
hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa
nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na
hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of
artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na
vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka
stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe
rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili
kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali
mapato.
80
Kwa kuwa yanahitajika maandalizi ya kutosha ikiwa ni
pamoja na kurekebisha sheria na kanuni mbalimbali,
utekelezaji wa hatua hii utaanza rasmi tarehe 1 Januari,
2013.
Tunaangalia uelewa wa wadau kuhusiana na hili na nini kifanyike ili kuweza kuboresha sheria husiaka ili iendane na taratibu na miongozo itakayoweza kuleta ukombozi wa kweli.
Kujua Zaidi Ungana na mwenzangu;TheImageProfession
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.
Music Festival 2012:Banana Zorro & B Band!!!!!!
B Band chini ya kiongozi mmiliki Banana Zoro ikitoa burudani ya moja kwa moja kwenye Tamasha kubwa la muziki wa dansi Tanzania lililofanyika kwa siku mbili tarehe 28 na 29 Septembe ,2012 ambalo lilishirikisha bendi mbalimbali maarufu katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
B Band chini ya kiongozi mmiliki Banana Zoro ikitoa burudani ya moja kwa moja kwenye Tamasha kubwa la muziki wa dansi Tanzania lililofanyika kwa siku mbili tarehe 28 na 29 Septembe ,2012 ambalo lilishirikisha bendi mbalimbali maarufu katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Wednesday, 19 December 2012
Mswahili Wetu Leo;SUSU COLLECTION BY SUBIRA WAHURE FOR SWAHILI FASHION WEEK 2012
Ni dada Mdogo mwenye mambo Makubwa!!!!!
Hizi ni Baadhi ya Kazi zake.Kujua Mengi kuhusu dada huyu ingia;http://subirawahure.blogspot.co.uk/
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima
Tuesday, 18 December 2012
Waswahili Na Maisha Yao;AFRICAN VILLAGE LIFE!!!
Waungwana; Leo tuangalie Maisha ya Kijijini..........
Jee wewe umewahi ishi kijijini?
Nini kizuri unakumbuka na Nini kibaya unakumbuka?.....
Jee Unafikiri kwanini Wazungu hupenda kuchukua Matukio ya Vijijini? kwa sababu ni mageni kwao,Wanataka kutusaidi au?.
MUNGU Ibariki Afrika,MUNGU Ibariki TANZANI!!!!!!!
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Sunday, 16 December 2012
Natumai Mlikuwa na J'Pili Nzuri;Burudani-Bado Sijafika - Kijitonyama Evangelical Choir!!!!
Wapendwa;Natumai Mlikuwa na J'Pili Njema.
Kama kuna iliyomwendea Vibaya Pole na Tambua MUNGU yu pamoja nawe na hajakuacha!!!!!!!!!
Neno la Leo;BWANA ndiye mchungaji wangu,Sitapungukiwa na kitu.ZABURI:23:1-6.
"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Sana.
Monday, 10 December 2012
Da' Mamie Msuya;Anawakaribisha kwenye MISA Ya mama Yake Mpendwa!!!
Mrs 'Mamie Msuya |
Familia ya Mr&Mrs Liberty Msuya inapenda kukualika/kuwaalika katika misa ya arobaini ya mama yao mpenzi; BULUNGU. (RIP) .
Itakayofanyika Jumamosi tarehe 15/12/2012,saa 8:oo Mchna[2:00pm].
katika ukumbi wa; Henley Green Primary School/Community Centre, Wyken Croft CV2 1hq.
Dress code black, white, or purple.
Kwa Mawasiliano Zaidi;07405389488[da'Mamie Msuya]
Ukipata Ujumbe huu wajulishe na wengine.
Asanteni na Karibuni Wote.
Sunday, 9 December 2012
Nawatakia J'Pili yenye Neema na Baraka;Burudani-Hellen Ken - Peleleza na Nyingene Nyingi!!!!!!
Wapendwa; nawatakia J'Pili yenye Neema,Baraka,Amani na Upendo.
Tena ndugu zetu,twawaarifu habari ya Neema ya MUNGU,Waliyopewa makanisa ya Makedonia;
Neno La Leo;2Wakorintho:8:1-15;Maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi,wingi wa furaha yao na umasikini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.
"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Wote.
Saturday, 8 December 2012
Chaguo La Mswahili Leo;African swagger - Alpha Featuring Rah P,No Maney.Twende Kazi,Nipo Poa.....Kazi Muruwaa za Waswahili!!!!!!!
Waungwana;"Chaguo La Mswahili Leo" Mmmmhhhh Motooo Afrika Mashariki Na Kati.....
Wewe tuu utuambie Video ipi imekubamba/kuipenda? Kwa nini?
Karibu sana....Swagger Swagger Swagger...........
"Swahili NA Waswahili" Motooooooooo.
Friday, 7 December 2012
Nderemo Na Vifijo kwa Kaka Frank Mungo'ngo' Na da'Levina Kimwaga!!![2]
Waungwana;ni Bwana na Bibi Mungo'ngo' sasa......
Picha za pamoja na Wazazi,Ndugu,Jamaa na Marafiki.
Bwana na Bibi Mungo'ngo' wanasema Asanteni woote, kwa Maombi/Sala,Michango,Kujumuika na katika Yooote.
Hawana cha kuwalipa bali ni kuwaombea kwa MUNGU awaongezee pale palipopungua na awalinde kila iitwapo Leo.........
Mtawasamehe kama kulikuwa na makwazo/kukosea,Haikuwa kusudi lao. kwani Binadamu hatujakamilika.
Wanawapenda Wooote!!!!!!!!!
Timu Nzima ya "Swahili Na Waswahi" na Wapenzi/Wadau Tunawatakia Masiha Mema.
Pamoja Daima.
Subscribe to:
Posts (Atom)