Jinsi ya kutengeneza maziwa
ya soya.
Baba
karudi ni makala fupi fupi ambazo zitakuwa zinatoa mwanga kwa jamii kujifanyia
mambo yahusuyo afya na maisha bora kwa ujumla wa ustawi wa jamii ya watanzania
kila wiki katika uwanja huu. Lakini la kufurahisha zaidi ni kuwa, hata kama
unakusudia kufanya kitu Fulani lakini hujui namna ya kufanya basi kutakuwa na
fursa kwako msomaji kutuletea maswali ambayo naahidi yatajibiwa yote ili
kuharakisha maendeleo ya Taifa letu. Uwanja huu utaitwa “Baba Karudi” ukiwa na maana nitakuwa natoa kile nilichopata katika safari zangu
duniani kote ambako shughuli yangu kubwa ni kukutana na wataalamu wa mambo
mbali mbali na kufanya mahojiano nao halafu nakuja kuwaletea watanzania wangu
hapa vile vile nitakuwa nayapeleka maswali yenu wasomaji juu ya yale mnayotaka
kuyafanya lakini hamjui yanafanywaje.. Nakuomba usiende mbali.
Leo
nimekutana na Bi Carole Bruzzano toka www.eHow.com. Nimefunga safari kuja Canada kupata ukweli juu ya
Soya kuwa maziwa safi na bora kwa afya za walaji. Yeye anasema:
Soya
inatumika duniani kote katika mapishi mengi mbalimbali ikiwemo kutengeneza
maziwa na kuungia kitoweo kama nyama na samaki au kama mbadala wa vitoweo hivyo
kiafya kwa mlaji.
Anasema
kutengeneza maziwa ya unga ya soya ni kazi ndogo sana ambayo inaweza
kukugharimu kama dakika 60 tu. Wenye viwanda vikubwa hupitia hatua nyingi
kutengeneza maziwa hayo ya unga ya soya. Lakini wewe unaweza tu ukatengeneza
mwenyewe nyumbani kwako tena kwa kutumia vifaa rahisi vinavyopatikana bila
kuazima kwa jirani.
Wewe unatakiwa
uanze na kuzisafisha soya kwanza, halafu weka juani zinyauke kidogo ili ngozi
ya soya ilegee na kasha umenye ngozi zote, uoshe tena na uzikaushe mpaka
zikauke kau! Hapo tayari utakuwa umeshaandaa soya kusagwa na kuwa maziwa ya
unga tayari kupeleka mahotelini na majumbani kwa matumizi.
Bi
Carole anasema unahitaji kuwa na vifaa hivi:
1.
Lazima
uwe na kikaango ili uzikaange soya zako kabla ya kusagwa.
2.
Unatakiwa
pia uwe na blenda au kinu cha kutwangia na chekecheke ili soya iwe unga laini
sana
3.
Mwisho
tayarisha vikombe viwili au vitatu vya soya
4.
Maziwa
halisi japo nusu kikombe kwa ladha na harufu.
Kaanga
soya yako katika kikaango angalia zisiungue.zikaange kwa dakika 10 hadi 15 na
utaona kuwa zimeiva kwa kubadilika rangi na kuwa kahawia basi ipua na ziache zipoe
kidogo kabla ya kuanza kuzisaga.
Saga
soya zako, chekecha mpaka upate unga laini sana, ukimaliza weka katika chombo
kikavu na kisafi. Sasa chukua maziwa HALISI nusu kikombe na tia katika soya
halafu changanya na anika mpaka mchangavyiko huo umekauka.
Mwisho
utaona unga umekauka lakini bado una madonge. Yapukuchue kwa mikono safi halafu tia soya katika mkebe safi tayari kwa
matumizi kama maziwa halisi.
Faida za
Maziwa ya soya
Unaweza
kuanzisha biashara ya kuuza maziwa kama wewe ni mama ntilie au una hoteli au
aina zingine za biashara ya vyakula na ukapata faida kubwa bila kuwa na
wasiwasi wa kupata hasara.
Maziwa
ya soya ni mazuri ukilinganisha nay a wanyama kwa kuwa hayana sukari asilia
iitwayo Lacoste ambayo sio nzuri kwa afya hivyo wenye aleji na maziwa ya
kawaida basi ndio muda wao wa kujidai na maziwa haya.
Maziwa
ya soya yana protini karibu sawa kabisa na ya wanyama lakini haya yana protini
ya mimea tofauti na ile ya wanyama ambayo si nzuri kwa afya. Protini ya mimea
ni nzuri mwilini kwa kuzuia upotevu wa calsiam kwenye mkojo na kukusaidia
usipatwe na magonjwa ya maumivu ya mifupa. Wenye kisukari ndio maziwa yao
haswa.
Maziwa
ya soya hayana mafuta yenye sumu (saturated fats) wala lehemu. Hivyo ni maziwa
yanayowafaa wagonjwa wenye maradhi ya moyo sana.
Maziwa
haya bado Bi Carole anadai kuwa ni kinyonya sumu mwilini kijulikanacho kama
“isoflavones” ambacho huzuia uzee wa kizembe, maraghi ya mifupa na kansa za
aina nyingi mwilini.
Mtu
akinywa kikombe kimoja cha maziwa ya soya basi ajue kuwa ana 20%ya isoflvones
ambayo katika maziwa ya wanyama hamna!
Hivyo
leo tunaishia hapa kwa kuwaasa kujitengenezea maziwa ya soya badala ya kuharibu
pesa ambayo ni ngumu sana hasa kwa kipindi hiki. Lakini pia tumefungua rasmi
ukurasa ambao tutautumia wasomaji kuuliza namna ya kufanya jambo lolote
ulitakalo. Wiki ijayo nitakuja na “JINSI YA KUJITENGENEZEA SODA YOYOTE” au kwa
lugha ya wataalamu ni “how to carbonated drinks” ambayo itatusaidia kupunguza
manunuzi ya soda kipindi hiki cha jua kali na pia tutaongelea faida na hasara
za kunywa soda pia.
Asanteni
kwa kunisoma na tuonane juma lijalo.
John Haule ni mpelelezi binafsi
(Private investigator) anayejihusisha na tafiti zenye suluhisho kwa matatizo ya
kijamii. Unaweza kumpigia kwa miadi ya
ushauri juu ya tatizo lolote linalokusumbua kibinadamu. Anapatikana Car
Painters - Temeke Stereo, Sandawe
Street, jirani na Dr. Massawe. Simu: 0768 215 956 au email rumoursafrica@gmail.com
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
No comments:
Post a Comment