Historia yake:
Kwa miaka
mingi sana nyama imekuwa chakula cha asili kabisa katika nchi yetu. Nyama
imekuwa ikiliwa na inaendelea kuliwa na vyakula vya wanga, na hapo ndipo nyama
ilikutana na jina jipya la kitoweo. Lakini pia nyama hailiwi tu kwa staili
hiyo, nyama pia ilijikuta ikipata jina lingine kwenye mabaa na vilabu vya pombe
iliposhushiwa na mafunda ya pombe na kuitwa asusa.
Nyama ni tamu
sana. Kuna uhakika wa kitaalamu kabisa unasema nyama ikipikwa au kuchomwa basi
utamu na mahitaji yake kiafya mwilini huongezeka mara dufu. Lakini nyama
ukiikuta mezani itakutatiza sana kujua hii ni ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, au
sungura. Vilevile inawezekana pia hata hisia zako zikawa tena mbali na ukweli
maana nyama ipo pia ya porini kama vile pofu, nyati, mbuni, swala, digidigi na wengineo
wengi tu, hivyo kuuliza kabla ya kula nyama ni muhimu sana hasa kwa wale wenye
miiko na baadhi ya vyakula na waislamu ambao baadhi ya nyama kwao
zimeharamishwa. Ila mimi nawaongezea jicho la tatu ndugu zangu hao kuwa
IMEHARAMISHWA tu lakini HAIKUKATAZWA kuila kama hutakuwa na jazba kunielewa
utagundua hivyo. Na mimi nafikiri leo naziharamisha nyama za aina zote hapa kwa
ushahidi wa madhara ya kiafya na kiroho pia.
Mungu pia hapendi nyama:
Kama
mtakumbuka mliosoma Biblia, Wajukuu wa Mungu Kaini na Abeli walijikuta siku
moja wakimtolea babu yao sadaka. Kaini akiwa kama mfugaji alichinja akamletea
Mungu nyama. Mungu alikataa na sadaka yake haikuteketea! Lakini Abeli akiwa
kama mkulima yeye alileta mazao ya shamba lake. Mungu alipokea! Ikawa Kaini akamwuua
nduguye Abeli na kizazi cha wafugaji kikajimegea dhambi ile mpaka leo.
Nyama inajenga matabaka:
Enzi zetu za
kujisomea hapa nchini kila nyumba ilikuwa na “Book Shelf” Leo zipo wapi? Sisi
tulisoma kitabu kilichoitwa UPUMBAVU WA MWAFRIKA na ndani kulikuwa na hadithi
nyingi tamu ikiwemo “Uchu wa Mzee Mikidadi” ambayo tulipoisoma tulielewa kuwa
nyama ina nguvu ya kuwagawa watu kimatabaka kwa uchu tu wa wenye madaraka,
ukiachilia mbali madhara makubwa zaidi ya kiafya.
Uharamu wa
nyama umeifanya jamii iwatenge wanyonge na kuwakweza wenye nguvu na mamlaka
katika kila Nyanja ya maisha. Angalia, Katika vitoweo vyote nchini na duniani
hakuna ambacho ni ghali kama nyama. Wanakula wenye pesa tu. Wapo akina mama wa
kambo walioripotiwa kuwalisha nyama watoto wao na kuwalisha maharage wale
watoto wa kambo. Katika jamii yoyote wenye mamlaka na nguvu ndio wanao faidi
nyama huku wengine wakiambulia mchuzi na mifupa. Ukiandaa sherehe usipoleta
nyama watu watakuwa hawakuelewi kabisa toka miguuni hadi utosini. Nyumba Fulani
Fulani nyama hupakuliwa na mama. Mboga za aina nyingine ni ruksa yeyote
kujipakulia. Wengine wameripotiwa kuwahesabia finyango za nyama wake zao. Wapo
pia wanawake waliopewa nyama kilo moja wapike ikafika mezani robo kilo tu,
lakini watu watakuambia wapo wanaume wanaokula kilo ya nyama wakiwa baa na huku
mke na watoto wanalalia uji. Huku utasikia mtoto kachomwa mikono kisa eti
kadokoa nyama, na mikasa kadha wa kadha inayotutahadharisha kuwa nyama itatutoa
roho!
Nyama inaua:
Lakini umeona
jinsi tulivyoiangalia nyama kwa historian a taswira tu bila kuiangalia madhara
yake kiafya ambayo ni lukuki kiasi hayaorodhesheki hapa leo. Nyama inatakiwa
iliwe kwa dharura tu na sio kama mlo kamili kwa kuwa nyama ina rekodi ya kuua
walaji wake kimya kimya bila wao kujijua kama wanateketea. Mfano watu mia
waliokula nyama kilo moja kila mtu kwa siku, watu 30 walikufa baada ya miaka
kumi na kuwaacha wengine taabani kwa magonjwa ya moyo kama kisukari, BP,
kupooza, ganzi n.k. Si hayo tu, bali magonjwa ya ini, figo na mapafu yalisababisha
vifo pia.
Unapokula
nyama unaongeza lehemu na mafuta yabisi mwilini ambayo hupenya na kuingia
katika mishipa ya damu na kuganda katika kuta zake. Kadiri mgando
unavyoongezeka ndivyo njia ya damu inavyopungua na mwisho kuziba kabisa! Sumu
hizo zinapoanza kuganda mgonjwa ataanza kuhisi matatizo na akipimwa atakuta
mapigo ya moyo yamefeli yaani BP. Kadiri atakavyoendelea kula nyama na kuziba
mishipa basi siku moja damu itapita kwa shida sana na ataanza kusikia ganzi
sehemu zote zisizopata damu. Mwisho mishipa ikiziba kabisa ndio huwa tunaita
mtu amepooza. Maana hakuna damu inayoenda huko tena! Dawa za wagonjwa hawa ni
kitunguu swaumu na mafuta ya Sardine toka Ueskimo tu. Kitunguu swaumu niliwahi
kukiongelea na nafikiri walionisikia wanaelewa cha kufanya. Ila haya mafuta ya
Sardine toka Ueskimo nitayaongelea siku nyingine.
Nyama inadhuru kisaikolojia pia:
Watu wa jamii
za wafugaji na walaji wakubwa wa nyama kwa ujumla ni wakorofi sana. Ni waoga na
wanaweza wakakudhuru bila kuwa na sababu za kutosha. Hawa jamaa wanaamini kuwa
kama huna silaha basi wewe si mwanaume. Hii imetokana na kujilundikia kiasi
kikubwa cha lehemu na sumu nyingine toka katika ulaji wa nyama uliokithiri.
Hupenda kulala wakiweka silaha kwenye mto ili wajiridhishe kuwa wanalala
salama. Kama ni hohehahe ataweka sime hata kisu tu, wakati mwenye pesa ataweka
bastola kabisa. Cha kukuchekesha msomaji wangu leo ni kuwa watu hao nchini
tumewapa “kibali baridi” cha
kutembea na silaha popote! Kama huamini toka wewe na jambia lako mkononi kama
utafika popote kabla polisi na watu wa usalama hawajakukamata. Utakamatwa kwa
sababu si sheria kutembea na silaha hadharani wote tunalijua hili, lakini hawa
ndugu zetu asili yetu imewakubali watembee hata na mikuki na hatuwaulizi
kulikoni.
Ikaja pia
staili mpya ya kuwaajiri kazi za ulinzi baadhi ya wala nyama hawa. Wenye akili
zetu tulibaki midomo wazi tukiamini staili hii itakufa siku si nyingi baada ya
wanaowaajiri kukutana na hasara ya kuibiwa kila kukicha. Na kweli leo hii
wamesahaulika… Mtu mwenye kiasi kikubwa cha lehemu mwilini ni mwoga, hajiamini,
na vitu kama hivyo kwa kuwa damu haitembei ipasavyo. Sasa mtu mwoga atalindaje
wakati yeye mwenyewe hajiamini na anatembea na silaha lundo! Yatakuwa maajabu
sana.
Madhara ziada ya nyama:
Lakini
madhara ya nyama bado hayaishi kama nilivyodokeza hapo awali. Kuna hili ambalo
sitaliacha. Ng’ombe, mbuzi, kondoo na mifugo mingine huwa wanakula chochote
kitamu kwao wanachokiona ardhini sote tunajua. Lakini tumeshuhudia wanyama hao
wakila nailoni, misumari, nywele bandia, na sumu nyingine nyingi tu
tunazozalisha binadamu. Sumu hizi tunakutana nazo tunapokula nyama na hakika
zinatudhuru vilivyo. Haya, Wanyama hao hao huwa tunawapeleka josho kuua wadudu
mwilini. Sumu ya zile dawa ni lazima ukutane nazo ukila nyama. Unalijua hilo?
Wachilia mbali sumu hizo, wanyama hupewa dawa wanapopatwa na maradhi tena dawa
kali (antibiotics) ambazo utazila na nyama na hatari yake ni kukujengea usugu
dhidi ya dawa za kibinadamu pale utakapougua. Ni hatari sana.
Kwa mila na
desturi zetu watanzania tuna nunua nyama pale buchani. Utakuta gogo moja
limevilia damu na ndilo linalotumika kukatakata nyama. Pale utajiuliza kwanza
usalama wa nyama juu ya lile gogo upoje maana hujui ni mti gani, una kamikali
gani, zinaua au ni salama na maswali mengine lukuki. Lakini ukimwuliza muuza
nyama hatakupa jibu lolote la kukuridhisha pale. Hajui. Upo mtaa Fulani wanaume
walikuwa wafanyakazi wa reli ambao walikuwa wakila nyama kwa wingi kuliko wake
na watoto wao. Leo hii mtaa hauna baba wote wamefariki. Kwa niaba ya watanzania
wote naishauri wizara ya afya kupitia mamlaka husika kuangalia uwezekano wa
kufunga misumeno ya kukatia nyama katika mabucha ya nyama maana ndio utaratibu
duniani kote na ndio ustaarabu. Vinginevyo kuna watu wanakufa kimya kimya.
Bado tu nyama
inaonekana ina maambukizi dhidi ya maradhi zaidi kuliko mboga za majani,
matunda na nafaka. Nyama hubeba wadudu wanaojulikana na wasiojulikana kila
unapoila kuja kukuambukiza maradhi ya aina mbalimbali.
Nile ua nisile nyama?
Lakini, nyama
bado ina utetezi wa kutosha kuwa na faida za kiafya. Msomaji wangu ona nyama
jinsi ilivyo shetani maana haieleweki kama tule, au tusile. Nyama hasa nyekundu
ni muhimu sana kwa afya yako lakini, inakubidi ule kidogo sana kama finyango
tatu tu kwa wiki, hiyo ni kitaalamu. Ukiifanya mlo rasmi utakufa! Cha ajabu
wakati vyakula vingine vikipikwa hupoteza ladha na uthamani wake, kwa nyama
mambo ni tofauti kabisa maana ikipikwa, ikichomwa, ikikaangwa ikiokwa nk ladha
huwa tamu ajabu na uthamani wake mwilini huongezeka mara dufu. Ukila nyama
unajipatia madini ya chuma, zinki, na protini kwa wingi mno.
Wengi wa
wagonjwa walioshindwa vitandani wanahitaji sana chuma, zinki na protini kuamka
na kupona haraka. Chuma humsaidia mtu kuwa na kinga dhidi ya maradhi sasa kama
hukupata virutubisho vya madini hayo basi unaweza kufa hapo kitandani kwa kuwa
hukula nyama mpaka chuma imeisha mwilini, hivyo usubiri ugonjwa utakaofuata
Anemia na baadaye kaburini. Mgonjwa huyu utamjua kwa dalili hizi: Kapoteza
uzito, ngozi imemkauka, mapigo yake ya moyo yanaenda mbio au taratibu sana,
Hana pumzi, kifua kinambana, kizunguzungu, hakumbuki tena kitu, kichwa
kinamuuma lakini sio malaria, miguu na mikono imekufa ganzi nk.
Usipokula
nyama pia tumesema utakosa madini ya zinki. Zinki pia ni kiboko kukupa kinga ya
mwili upambane na maradhi sasa kama hamna lazima maradhi yakulaze kitandani.
Wanandugu mpeni virutubisho vya zinki kabla hamjampoteza ndugu yenu. Mkitaka
kumjua kuwa anahitaji zinki angalieni yafuatayo: Mgonjwa hana utulivu na usiku
hapati usingizi, kama ana vidonda haviponi, ana vidoadoa au alama ya nusu mwezi
katika kucha zake vidoleni, anakosa nguvu nk. Ukiona dalili hizo hebu wahi umpe
virutubisho vya zinki apone vinginevyo mtamkosa.
Lakini pia
usipokula nyama unajikosesha protini. Protini ikipungua mwilini utaona mgonjwa
anapata tabu kupona vidonda, analalamika viganja vinawaka moto, analalamika
miguu inamuuma na muda mwingine atasema tumbo pia linamuuma mara kwa mara, hana
nguvu, anashambuliwa na maradhi ya ngozi na wengine hukonda vibaya.
NATIVA ni suluhu:
Hapa Tanzania
kuna virutubisho vya kurejesha afya ya mgonjwa huyo haraka na salama. Makampuni
mengi yapo kiushindani katika biashara hiyo kila mtu akikushauri kutumia zake.
Mimi kwa uzoefu wa maradhi haya nakuelekeza msomaji wangu tumia virutubisho vya
kampuni ya NATIVA toka Afrika Kusini kama unatafuta suluhu ya uhakika na haraka
kwa mgonjwa wako. Nativa wapo mji mzima na ukihitaji dawa nipigie tu simu
nitakusaidia kuzipata.
Wapo wakulima
ambao si wafugaji nap engine kupata nyama si kitu rahisi. Kizazi cha Abeli
yaani Wakulima wao madini ya chuma, zinki na protini wamejaziwa kwenye mazao
yao hivyo utavipata vitu hivi ukila mboga za majani, karanga na jamii yote ya
njugu, maharage na jamii zake, matunda kwa wingi nk. Hivyo hakuna sababu ya
kungoja upungukiwe na madini hayo mwilini.
Kula nyama
msomaji wangu. Lakini usiigeuze kuwa mlo rasmi, kula kama waislamu
walivyoambiwa katika msaafu kuwa nguruwe ni haramu aliwe kwa dharura tu. Lakini
mimi leo nakuambia wewe kula nyama yoyote kwa dharura tu. Kama Mungu
alimkatalia mjukuu wake Kaini sadaka ya nyama aliyomtolea jiulize nyama ina
nini?
Bwana pori
mmoja alisema hivi: Baba anayekula nyama kwa wingi anajijengea uhayawani wa
ndege na wanyama wanaowala wenzao (predetors) msituni. Na ndio maana huwa baba
wa aina hii huzinyanyasa familia zao…
Kama umekula
nyama kwa muda mrefu na unajihisi dalili zilizopo hapo juu tafadhali
tuwasiliane nikusaidie. Kama una mgonjwa wa kisukari, kupooza, presha zote,
kupungua na kuzidi uzito pamoja na dalili za maradhi kwa kukosa madini kama
nilivyoorodhesha hapo awali basi usisite kunitafuta ili nikupe dawa za uhakika
upone.
Asanteni sana
kwa kunisoma na mungu awabariki sana.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.
3 comments:
nimerudi Kachiki nikitengamaa nitasema zaidi..nimeipenda picha yako hapo juu:-)
Wawo wawooooo "Kadala" Tunashukuru kwa kurudi salama!!!!Sande bhehhh..
Nilikumithiiii...ukisha pumzika na ukiwa nyumbani nitumie sms!! nikupigie tulongane......
Wasalimie woote hapo Nyumbani na msimalize hizo thawadiiii
nashukuru sana kwa ujumbe wako mzuri sana ulotuandikia hapa kuhusu madhara ya nyama.
Ila kwa ufahamu wangu mdogo wa biblia nadhani hapo umechanganya kdogo ebu karudie tena kusoma kipengele kile cha Kaini na Abeli, sadaka ya Abeli ilikua ya nyama na ya Kaini ilikua ya mazao, kwa kumbkmbu zangu Kaini altoa masalia ya mazao yake lkn Abeli alitoa uzao wa kwanza wa wanyama wake tena alitafuta walionona sana na sadaka yake ilikubaliwa moja kwa moja lkn ya Kaini ilikataliwa sababu alitoa kwa kinyongo na dharau.......
ni kweli nyama ina madhara kama ulivotueleza lkn kwa hapo kwny bible naomba urudie tena pls ni ktk kukumbushana tu.
Asante sana na kazi njema
Post a Comment