Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 20 January 2013

Wapendwa Nawatakia J'Pili Yenye Ushindi;Burudani-Geraldine Oduor - Wewe ni Mungu na Nyingine Nyingii!!!


Wapendwa Poleni na Snow natumaini hamjambo na kufurahia majira aliyoyaweka MUNGU na kushangilia. Ikiwa snow kama Greenland  Mchanga na Joto kama Sahara Baridi kama Himaya Mvua na Radi za Ikweta.Tusilalamike Nawatakia Kila la Kheri.....

Ujumbe huu  Wa kutia Moyo Nilitumiwa na Kaka yangu ALEX LUKUNDO Wa hapa COVENTRY .


Nami nimependa kushiriki nanyi  NA Kuongezea....Hasa mliokuwa kwenye Hali ya hewa kama hii isiwe sababau ya kukosa Kushiriki IBADA.




Wapendwa Muwe na J'Pili Njema, Yenye Unyenyekevu,Upendo,Busara ,Ushindi na Shukrani.Msijiwekee hazina duniani,nondo na kutu viharibupo,na wevi huvunja na kuiba;

Neno La Leo:Mathayo Mtakatifu:6:19-21;Kwakuwa hazina yako ilipo,ndipo utakapokuwapo na Moyo wako.

          "Swahili NA Waswahili" MUNGU Awabariki Sana.

5 comments:

emuthree said...

Na j3 njema ndugu wa mimi TUPO PAMOJA

Yasinta Ngonyani said...

Duh! hii baridi nayo ..naona huko si wazoefu sana wa baridi..LOL haya jumapili njema kachiki waz mimi:-)

Mija Shija Sayi said...

HEEEEEEE!!!! Ulaya Ulaya Tu..

Rachel umewiva balaaa hasa hiyo picha ya kufunga macho..

Rachel Siwa said...

Asanteni sana wapendw....

@Da'Mija......hoiiiiiiiiiii...niongezee wale Dagaa kama bado wapo dadangu..NIMEJINYANYASAAA Nimechemka..

Mija Shija Sayi said...

hahaaahahaa...ntakuongeza usihofu kabsaaa mdogo wangu..