Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 30 January 2013

Watoto Na Mitindo;Pata na Video Hairstyle Slideshow!!!!


Aliye msuka huyu  ndiyo aliyekuwa akiwasuka watoto wangu..Nimefurahi kusikia bado yupo na anaendelea vyema na kazi zake kwa watoto...tena anawezana nao haswa...

Waungwana; Mimi naamini watoto wana Mitindo yao..pia wakipendeza wao wenyewe na wazazi tunakuwa na furaha sana..

Si Lazima au si wote wanapenda  watoto wasukwe..basi hata kama ana Nywele fupi..kuna Vibanio vyao pia wanapendeza sana......

Nao Watoto  kuna Umri wewe mzazi utamchagulia Mitindo ya Nywele lakini kuna Umri mwingine Mmmhh !!...inakuwa kazi ya ziada, Yeye/Wao hutaka hivi nawe unataka hivi..basi ni mabishano tuu..kama wapo wawili huwa wanaangaliana wao na kucheka au kuguna....hahahhaahhah imeshakukuta hii?

Karibuni sana kwa Maoni/Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.....

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.





6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Binasi kwa kweli sijui niseme nini kwani mimi napenda kumwacha mtoto kama mtoto ...ila hii ni mimi..na nimeona hapo wanapendeza kwelikweli

Rachel Siwa said...

Asante da'Yasinta, lakini yule ananywele ndefu..sasa wakati zinakuwa japo nywele zake si za kukaa muda mrefu akisuka..

Jee ulikuwa unaziachaje/ unafanyaje yaani anachana tuu mpaka zinakuwa?

Anonymous said...

NAMUUNGA YAHSINTA ,HATA MIE NI MAMA MWENYE WATOTO 2 .WAKIKE NA KIUME .MTOTO WANGU WA KIKE HUMBANA TU .NAPENDA MTOTO AONEKANE MTOTO . HUWA NAONA AJABU MTOTO NA RASTA LIPSTIK,WANJA, TUWALINDE WANETU TUSIWAFANYE VIVUTIO BADO WADOGO YOTE WATAYAKUTA

Rachel Siwa said...

Asante sana Mzazi..kwa Maoni yako..na karibu sana.

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki!..haswaaa ni kuchana tu na kubana ..swala la kusuka mmmhh hapendi kabisa labda kwa vile sikumzoesha tangu udogodogo..

emuthree said...

Tabia na makuzi ya mtoto yanatokana na wewe mzazi.....oh, Tupo pamoja mpendwa