Kila mtu anapenda kuwa na furaha muda wote, Ila kwa bahati mbaya sio wote tunafuraha kwasababu mbalimbali za kimaisha. Wengine wana matatizo ya kiafya, wengine wana matatizo ya kiuchumi na wengine wana matatizo ya kimahusiano na watu muhimu kwao, yote haya ni matatizo tunayokabiliana nayo katika maisha. Licha ya kuwa kila mtu na matatizo yake bado kuna maana na umuhimu wa wewe kuwa na faraja ya kuwa hali za maisha yetu hubadilika kila siku. Hakuna hali isiyobadilika iwe nzuri au mbaya ila tuna matumaini ya kuwa siku zote tuwe wenye furaha na mafanikio katika pilikapilika za maisha yetu. Kwa mantiki hiyo kuna mambo ambayo ukizingatia yatakuza na kuimarisha furaha yako.
Je ni mambo gani hayo?
Inaendele..Zaidi ingia;http://kamotta.blogspot.co.uk/
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
1 comment:
Ni kweli mpendwa, baada ya dhiki ni faraja,..tusikate tamaa na madhila, matatizo..kwani yote ni mitihani ya kimaisha...tupo pamoja mpendwa
Post a Comment