HUKU JIKONI MAMBO YANAPAMBA MOTO:Sasa tunapatikana ndani ya ……………
Leo ni siku ya furaha hapa jikoni na naamini itakua siku ya furaha kwa wanafamilia wote wa jiko hili. katika kufurahi huku basi hata wale ambao si wanafamilia wa jiko hili watavutiwa kujiunga nasi.
Lakini kabla sijakwambia kulikoi ya furaha hii, nachukua nafasi hii kukushukuru wewe mwanafamilia wa jiko hili kwa kuwa nasi kila siku hapa jikoni. Uwepo wako jikoni hapa ndion chachu ya maendeleo ya jiko hili.
- Mchango wako ni wathamani sana kwetu , unaposoma makala zetu, unapoandika comment, unapo like page , unapo tu-follow kwenye twitter, Unapotutizama kwenye instagram , unapotutumia barua pepe, unapo tupigia simu au unapowaambia wengine juu ya jiko hili unakua umechangia sana kuliendeleza jiko letu.
Waswahili husema HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA, wenzetu waingereza husema A JURNEY OF A THOUSAND MILES BEGINS WITH A STEP. Jiko letu pia lilianza kama mchicha,na kadri siku zinavyozidi kwenda nasi tunakua na tunazidi kuongezeka. Ninakila sababu ya kuamini kwamba hapo mebeleni familia yetu hapa jikoni itakua kubwa sana.
Furaha ya familia ya jiko hili leo inaletwa na hatua moja kubwa ambayo jiko letu limepiga. Kwa mara ya kwanza kabisa jiko hili limeweka VIDEO YAKE YA KWANZA NDANI YA YOUTUBE. Link ni hii, bofya http://www.youtube.com/watch?v=zpTnpAljBd0
Kwa kua ndio video ya kwanza, basi tuliona nivyema iwe video ya kuitambulisha Tollyzkitchen kwako. Tunaamini ukilifaham jiko hili vizuri basi utapata sababu ya kukaribisha na wengine. Na pengine utapenda kuungana nasi katika shughuli mbalimbali za hapa jikoni.
Hapa jikoni tutarusha video za aina tatu ,
- Makala maalum za maongezi tu (kama hii unayotizama leo). Makala hizi zitakua ni mtiririko wa maongezi au mafundisho juu ya mambo mbalimbali ya jikoni.
- Makala za mapishi kwa vitendo. Hizi ni video ambazo zitafundisha na kuelekeza namna ya kupika vyakula mbalimbali pamoja na mambo mengine ya jikoni.
- Makala maalum za mahojiano. Haya yatakua ni mahojiano juu ya mambo mbalimbali yanayohusu chakula na yanayokizunguka chakula.Hapa utawasikia watu mbalimbali kama wajasiriamali, wakulima, wanasiasa, masupa staa na wengine wengi.
Makala hizi zote zitakua katika lugha ya Kiswahili. Unapozitafuta ndani ya YOUTUBE pia tumia vichwa vya habari vya Kiswahili,kama utatumia jina basi fatuta TOLLY BEN. Hata hivyo Tutajitahidi sana kuweka link zote kwenye blog ili kukurahisishia .
Nakuomba sana na nakusihi uwakaribishe na wengine jikoni hapa, makala hii yakwanza ikikufurahisha itakua vyema sana uki share link hii na wengine.
Naamini taarifa hizi ni njema kwako na zimekufurahisha kama ambavyo zinatufurahisha sisi hapa jikoni.
TOLLYZKITCHEN TUNAPORESHA MAPISHI NYUMBANI
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
No comments:
Post a Comment