Wapendwa/Waungwana..Tarehe kama ya Leo,Mwezi kama huu,Siku kama hii Alhamisi ..Familia ya Bibi na Bwana Kiwinga,MUNGU aliwajaalia mtoto wa kike mwenye Afya Njema.
Leo ni kumbukumbu ya Siku yangu ya kuzaliwa, na imejirudia kama ilivyo kwa siku hii ya Alhamisi..
Na Rudisha Shukrani na Utukufu kwa MUNGU BABA MUUMBA.Yeye ananijua zaidi ya wote,Yeye amenifanya hivi nilivyo,Yeye ameniokoa na kunilinda siku zote,Yeye ni Faraja yangu katika maisha yangu,Yeye ni Dereva wangu,Yeye ni Mwalimu wangu,Yeye ni Mwamba wangu,oohh MUNGU wewe ni kila kitu Maishani mwangu,Unatoshaa BABA..Wewe ukisema ndiyo nani atasema siyo?
Shukrani; kwa Wazazi/Walezi kwa yote.Nathamini na kukumbuka meengi sana sana hasa pale ninapo kutana na Mapito/Majaribu,Furaha na Kupiga hatua mpya.Sauti zenu haziishi masikioni Mwangu,Maneno yenu/Wosia,Upendo ,Ukarimu na Faraja zenu..Sina lakusema zaidi ya Asanteni na nawaombea kila iitwapo Leo na kuwapenda Saaaana.
Shukrani; kwa Mume wangu kipenzi kwa yote,wewe ni mwanaume unaye faa kuitwa MUME/BABA,Sijilaumu wala Kujutia kamwe kuungana nawe.MUNGU asante kwa Ubavu huu wangu.
Shukrani;Watoto wangu wote,Dada zangu na Wadogo zangu,Kaka zangu wote,Mawifi,Mashemeji.
Shukrani;Ndugu,Jamaa,Marafiki, kwenye Safari ya Maisha yangu nimekuta na Ndugu,Watoto,Dada,Kaka .Ambao si wakuzaliwa nao katika Tumbo Moja/kutokea Ukoo mmoja,Lakini kwangu nawathamini sana sana na Nawapenda mnooo.Ni vigumu kutaja kila mmoja lakini wenyewe manajijua.
Shukrani; Blogger wote,Wapenzi/wafuatiliaji wote wa Swahili na Waswahili,Mitindo Afrika na Nga'mbo,Watoto na Jamii.Pamoja Daima.
Nichukue Fursa hii kukuomba Msamaha/Radhi kutoka moyoni ,Wewe niliyekukosea,kwa makusudi au bila ya kukusudia,Nilikukwaza,kukuletea /kukuingiza majaribuni.
Nami nichukue Nafasi hii kwa Kuwasamehe wale wote walionikosea/kunikwaza.MUNGU BABA Na atusamehe Sote!!!!!!!
Asanteni kwa mlionitumia ujumbe,Mlionipigia simu,Mlionitumia/letea zawadi,Mlioniombe/endelea kuniombea Sala/Dua zenu nimezipokea.
Nikisema niendelee hapa sitomaliza mpaka kunakuchaa..kwani kwa umri huu nimepitia Meengi,Ngoja niishie hapa na Mengi usome:1.Wakorintho:12:1-31.[15]Kwa maana mwili si kiungo kimoja,bali ni vingi.
Asanteni sana kwa Kunisoma na MUNGU awabariki Nyote!!!!
Ni mimi;Rachel-siwa.
"Swahili na Waswhili"Pamoja Daima.
7 comments:
KACHIKI WA MIMI HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA LEO...Mwenyzi Mungu akujalie miaka mingi mpaka uwaona wajukuu na vitukuu.ni mimi Kadala
HONGERA SANA MPENDWA, NDUGU WA MIMI, MUNGU AKUPE AFYA , BARAKA NA MAISHA MEMA,...NA BLOG YA DIARY YANGU INAUNGANA NA WEWE KWA KUSEMA `HAPPY BIRTHDAY TO YOU'
Happy birthday
Amee!!Amee!!! Asante sana KADALA wa mimi..Pamoja sana.
Amneen!!Ameee!!!!!Inshaallah Ndugu wa mimi na timu nzima ya DIARY YANGU..Pamoja Daima..
Thanks..@Anonymous.
Hongera sana Mdogo wangu kwa kutimiza miaka.. Mungu wetu azidi kukupa miaka mingine mingi yenye furaha na afya tele.. Amen!
Daah! nilitaka kusahau umefikisha mingapi madame...lol??
Ameee!!!!Asante sana dadake..uwiii yaani kweli ulezi umekushinda..yaani ile kadi ya kiliniki umeshaitupa?...Maisha ndiyo yameanza MADAME.....
Post a Comment