Waungwana; Jukwaa La Mashairi.Jukwaani Leo na Mshairi,Mswahili wetu ; Prof.Ahmed Nabhany, Anatuchambulia tofauti ya Mashairi.
Wewe unapenda Mashairi? ni Mtunzi /unajua Mashairi,Ngonjera au?
Karibu Sana.......
"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.
2 comments:
Mimi ni mtafiti wa miaka mingi wa tungo za zamani za ki-Swahili. Na katika shughuli hizo, nimebahatika kukutana na Ustaadh Ahmed Sheikh Nabhani mara kadhaa, kupata utaalam na uzoefu wake.
Ni mtaalam wa tungo hizo, na pia yeye mwenyewe ni mtunzi mahiri sana. Ingawa yeye hakusoma chuo kikuu, hakuna msomi wa chuo kikuu chochote anayemfikia. Badala yake, wasomi maarufu kutoka kote duniani amewafundisha na bado anawafundisha. Wanamtembelea kwake Mombasa au wanamwalika kwenye vyuo vyao, iwe ni u-Jerumani, Marekani, na kwingineko.
Huyu ni kati ya wale wazee wa ki-Swahili ambao elimu yao ya taaluma ya kiSwahili, iwe ni tungo au lugha, ni ya kiwango cha juu mno. Ukija Tanzania, unawakuta mabingwa wengine kama Amiri Andanenga wa Tanganyika, na Haji Gora Haji wa Zanzibar.
Jambo muhimu tunalopaswa kufanya ni kusoma na kuyatafakari maandishi ya mabingwa hao, kuandika vitabu na tasnifu juu yao, kufanya nao mahojiano zaidi, ya kina na upana, ambayo hayaweza kuisha, bali ni jukumu la miaka na miaka.
Inatisha kuwa jamii yetu haina nidhamu ya namna hiyo. Nenda chuo kikuu chochote cha Tanzania uone kama kuna mtaalam anayetambulika kimataifa wa tungo za Ustaadh Ahmed Sheikh Nabhani, au Andanenga au Gora Haji Gora.
Nenda uona kama kuna yeyote ambaye ametumia miaka na miaka kuyatafakari maandishi, maisha, na falsafa ya mabingwa hao.
Tukubali kwamba hatuko makini.
Asante sana PROF.MBELE. Umenipa/Kutupa mwangaza zaidi juu ya Ustaadh Ahmed na Tungo zake..Pamoja na Mabingwa wetu wa kujivunia kina Amiri Andanenga na Haji Gora.
Tuendelee kujifunza.
Post a Comment