Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 28 February 2014

[AUDIO]: Mjadala kuhusu Mitandao ya kijamii kutoka Jamii Production


Karibu katika kipindi hiki cha kwanza cha moja kwa moja (Live) kilichorushwa toka studio zetu za Washington DC

Katika kipindi hiki, mjadala ulikuwa juu ya MITANDAO YA KIJAMII.

Washiriki walikuwa Prof Nicholas Boaz. Mwalimu wa Mawasiliano kutoka Chuo kikuu cha Maryland.

Mzee
Emmanuel Muganda. Mtangazaji mkongwe aliyefanya kazi zaidi ya miaka 30
katika Idhaa za Sauti ya Amerika (VOA) na pia Denzel Musumba. Mmiliki wa
Border Media Group ambaye kwa miaka mingi amekuwa akitangaza kupitia
mitandao ya kiJamii

Kwa njia ya Skype tuliungana na Jeff Msangi. Mwandishi, Blogger na mwanaharakati aliyejiunga nasi kutoka Ontario Canada


Na kutoka nchini Tanzania tulimsikia mwakilishi wetu Ahmad James Nandonde aliyeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mara na watu wengine.

Karibu sana



NB: Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa sauti katika baadhi ya sehemu za kipindi.

No comments: