Waungwana;"Jikoni Leo",Tukumbuke vifaa hivi vya kupikia na Kuhifadhia/Kuwekea Maji ya Kunywa.
Mimi navijua kama Vyungu/Chungu na Mtungi.
Wewe unavijua kwa jina gani?
Jee Umewahi /Bado Unatumia?
Mtoto wangu Sandra Alipokuwa mdogo alikuwa anaita Vyungu/Chungu.."KIMBONDO"
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
3 comments:
Yaani KACHIKI...si unakumbuka chakula cha kupiga kwenye chungu kinavyokuwa kitamu..na Maji ya kwenye mtungi yanvyonoga..Nilipokuwa Matema Beach nilifika mpaka kule wanakotengeneza mitungu/vyungu na vyombo vinginge mbalimbali nikanunua mtungi natunzia maji ya kunywa..kinachokosekana ni KATA YA KUNYEA...AHSANTE KWA KUMBUKUMBU...
Kabisaa KADALA.....Jee Mitungi/Vyungu unavyo hapo au umeacha Ruhuwiko?
Kama ndio Mtungi ulifika Salama?
Aminia KADALA wa mimi...
Kwa Kiongoni Vinaitwaje?
Usikonde KACHIKI nitakuwekea picha ninavyo hapa ..:-) NA NITAKUAMBIA KWA KINGONI TUNASEMAJE KAZA MOYO:-)
Post a Comment