Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 22 March 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90: Kupotea kwa Air Malaysia na takwimu za usalama wa anga duniani‏

Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011.
Photo Credits: PressTv
Wakati harakati za
kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi kushika kasi
na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya takwimu
kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na kufungua
macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na / ama
miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.


Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network
ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya
dunia.



Kwa mujibu wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea
tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa ndege zinazopotea na kutopatikana
wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.


Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90
ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es
Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30
AM).

No comments: