Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 28 April 2014

Mhe Mwigulu Nchemba akizungumzia suala la uraia pacha Washington DC‏

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akihojiana na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production Washington DC.

Photo Credits: Habari Kwanza blog
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa anajivunia kiasi cha UZALENDO walichonacho waTanzania hapa nchini, jambo linalompa moyo kuendeleza harakati zake za kusaidia kupatikana kwa uraia pacha, ombi lililo kuu kwa waTanzania waishio nje ya nchi katika mabadiliko ya katiba mpya.

Mhe Nchemba, ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika jijini Washington DC nchini Marekani, amesema kuwa ushiriki wa waTanzania na rafiki zao katika maadhimisho haya, umemdhihirishia nia na mapenzi yao kwa nchi yao, na hilo limemsukuma zaidi kusaidia kupitishwa kwa suala la uraia pacha kwenye katiba mpya.

Hii ni ripoti katika kipindi cha Morning Jam

Hotuba Ya Mhe. Mwigulu Nchemba katika sherehe za Muungano Washington DC‏


Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza katika moja ya hafla hapa Washington DC
Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog
Ifuatayo ni hotuba ya Mhe Mwigulu Nchemba.

Naibu Waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Tanzania Bara) aliyoitoa katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano hapa Washington DC.

Audio hii ni kwa hisani ya Vijimambo Blog


Sunday, 27 April 2014

Muendelee Vyema na Jumapili Hii Iwe Yenye Maono Na Imani;Burudani-Upendo Group Kijitonyama - Mungu Anakupenda,Sifa na Zivume!!!!

Wapendwa,Natumaini J'Pili hii inaendelea vyema,Na iwe Yenye Imani,Maono/Ndoto,Shukrani na Hekima.
Mithali:29:18;Pasipo Maono,watu huacha kujizuia;Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.


Neno La Leo;Waebrania:11:1-40.[Maana Ya Imani]
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,ni bayana ya mambo yasiyoonekana.






"Swahili Na Waswahili"MUNGU Atubariki Sote.

Friday, 25 April 2014

Maandalizi ya sherehe za Muungano Washington DC‏





Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akizungumzia maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya muungano ofisini kwake Washington Dc Jumatano, Aprili 23, 2014.
Photo: Sunday Shomari

Thursday, 24 April 2014

Mswahili wetu Leo;Da'Faiza wa Fabuloustaa!!!!!!!

Mswahili wetu Leo ni  da'Faiza Omar.
Binti huyu ni Blogger na ana mambo meengi mazuri
Kumjua zaidi Karibu sana kwenye Blog yake.

Mtembelee hapa;http://fabulousfaa.blogspot.co.uk

Tuesday, 22 April 2014

Mazungumzo na Dr Patrick Nhigula kuhusu Bunge maalum la Katiba‏





Karibu katika mazungumzo na Dr Patrick Nhigula kuhusu mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.
Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu suala hili muhimu kwa mustakabali wa nchi ya Tanzania.
Karibu

Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

Saturday, 19 April 2014

Shukrani/Asanteni Wote na MUNGU awabariki Sana!!!!


Salaam Waungwana;

Tunamshukuru MUNGU mwenyeezi kwa yote.
Tunamshukuru MUNGU kwa maisha ya Mama/Bibi yetu mpendwa Khadija Mgaya Chuma[bibi Mwalimu].
Tunamshukuru MUNGU kwa kufanikisha vyema,Mazishi ya Mpendwa wetu.
Bi Khadija alifariki usiku wa Jumanne na Kuzikwa siku Alhamisi katika Makaburi ya Ilala Mchikichini.Dar.
Mama Kiwinga na Familia yake,Wanawashukuru sana Ndugu,Jamaa,Marafiki,Majirani na Wote walioshiriki kwa Michango,Muda,Upendo,Faraja, Sala/Dua na Mengineyo.
MUNGU azidi kuwabariki na kuwaongezea kila lililo jema kwenu.

Wenu Mama Kiwinga
Wa Ilala Sharifu/Shamba.

Asante Sana.


"Swahili Na Waswahili" Tunawashukuru wote katika yote.

Sunday, 13 April 2014

Nawatakia JumaPili Njema;Burudani-Molimo na Nzambe yaka/Nitakushukuru,Mungu ni mwema/Kombo nayo ekumama ,Kutoka kwa- Feza Shamamba Hosseya

Wapendwa;Nawatakia JumaPili yenye Unyenyekevu,Upole,Uvumilivu,Upendo na Umoja....

Kwahiyo nawasihi,mimi niliye mfungwa katika BWANA,Mwenende kama  inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;
Kwa unyenyekevu wote na upole,kwa uvumilivu,mkichukuliana katika upendo.

Neno La Leo;Waefeso:4:1-16
3.Na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
4.Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
5.BWANA mmoja,imani moja,ubatizo mmoja.
6.MUNGU mmoja,naye ni BABA wa wote,aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
7.Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. 






"Swahili Na Waswahili"MUNGU Atubariki Sote.

Saturday, 12 April 2014

[AUDIO]. DAKIKA 90 ZA DUNIA: Maadhimisho ya Kwibuka20, Washington DC‏


 Wiki
kama hii, miaka 20 iliyopita, nchi ya Rwanda ilishuhudia kuanza kwa
mauaji ambayo kwa siku 99 zilizofuata, yaliacha historia mbaya na ambayo
itaendelea kukumbukwa na vizazi vijavyo.
Ndani ya siku 100, watu wanaokadiriwa kufika milioni 1 waliuawa katika mauaji ya kimbari.
Miaka
20 baadaye (mwaka huu), dunia nzima imeungana na Rwanda kukumbuka kile
ambacho wengi wanaona kuwa kilitokea na kuachwa kuendelea kutokana na
Jumuiya ya kimataifa kutoingilia kati na kutoa msaada muafaka kwa wakati
muafaka.
Kumekuwa na matukio mbalimbali kukumbuka mauaji ya kimbari
ya Rwanda ambayo yamefanyika duniani kote, Kutoka Kigali Rwanda mpaka
hapa Dar-Es Salaam na hata huko Washington DC.



Hii ni sehemu ya
ripoti ya Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA
kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Friday, 11 April 2014

Jikoni Leo;Kitchen Boss- Date Night Dessert,Buddy and wife Lisa..!!!!!

Waungwana;"Jikoni Leo" mimi huwanafuatilia/Mpenzi Sana wa  vipindi vya huyu Bwana..Basi leo nikaona vyema nikusogezee hapa, kama wewe hujapata kuviona Au ulipitwa na hiki au kingine basi upate uhondo kidooogo....

Mwanaume Jiko au?

Mwanaume akipenda jiko/kupika  wengi wao wanakuwa wapishi wakubwa na kuwa kazi na yenye kumuingizia Pesa.Lakini Wanawake wengi ,wapishi wanaishia kupikia familia, mitaani/mama Ntilie.... ni wachache sana inakuwa kazi ya Maana/kumuingizia pesa. Hivi ni kwanini?


"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Tuesday, 8 April 2014

Maangalizi ya afya Washington DMV...bure‏



Wataalam wa afya DMV (HCP Metro DC) wanatuleta huduma ya afya kwa wale wasiokuwa na bima ya afya. Huduma hii itatolewa kwa usawa bila kujali dini,rangi,umri,uraia au uchumi.



Kama una rafiki, ndugu au  mzazi asiyekuwa na bima ya afya tunaomba mshiriki ili tuwe na jamii inayoshamiri na yenye afya njema. Zoezi hili litachukuwa hatua ya kuwaona wale watakaokuwa na hali pungufu ya afya njema mara moja kwa mwezi.




Tarehe: 04/12/2014   (Jumamosi)
Saa 3:00 asubuhi hadi mchana 7:00 (waweza kuja hata kwa saa moja)  
MAHALA
3621 Campus Drive, 
College Park, MD 20740

Leo hii wadau wetu tunaomba tujitolee kufanikisha huduma hii ya maangalizi ya afya ya bure kwa wadau wa DMV. 

Unaweza kujitolea kwa namna mbalimbali


  • Iwe ni kumsadia mtu usafiri,
  • kuandikisha majina ya wanaokuja
  • kubeba na kupanga meza kabla na baada ya maangalizi
  • au kushiriki katika timu ya kitaalam
Tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe nesiwangublog@gmail.com ili tuweze kupata idadi na uhakika wa msaada wako.

Monday, 7 April 2014

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA. Mauaji kwenye kambi ya jeshi Fort Hood‏

Jenerali Mark Milley, Kamanda wa Fort Hood akizungumza na waandishi wa habari  
Wiki iliyopita, nchi ya Marekani ilikumbwa na mauaji mengine yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi huko Fort Hood, Texas.

Jumatano Aprili 2, askari mmoja wa Jeshi la nchi hiyo, Ivan Lopez ambaye
inasemekana alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo, aliwafyatulia
risasi na kuwaua wanajeshi wenzake 3, kujeruhi 16 kabla hajajigeuzia
bastola na kujiua

Mauaji haya, yanarejesha kumbukumbu ya mauaji
makubwa kabisa kutokea kwenye kambi za jeshi nchini humo, yaliyotokea
kwenye kambi hiyohiyo takriban miaka 5 iliyopita.



Hii ni sehemu ya
ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA
kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Sunday, 6 April 2014

Tumalizie JumaPili hii kwa Amani;Burudani-PASTOR ANTHONY MUSEMBI - Unastahili na ni Wewe,Mataifa Yote,Unaweza,natamani Wamebarikiwa,Nakuabudu Na Angalia.!!!!!

Wapendwa;Nimatumaini yangu JumaPili hii Imeenda/inaendelea Vyema...Muwe na Amani,Baraka,Rehema, na Upendo

Mwanangu,usiisahau sheria yangu,Bali moyo wako uzishike amri zangu.


Neno La Leo;Mithali:3:1-10
Rehema na kweli zisifarakane nawe;Zifunge shingoni mwako;Ziandike juu ya kibao cha moyo wako
.




Mmmmhhhhh..MUNGU ni MWEMA SAANA.


"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Wote Mliopita Hapa.

Wednesday, 2 April 2014

Wa Afrika Na Sherehe zao Leo Tupo ;RWANDA: TWIN BROTHERS MARRY TWIN SISTERS!!!!!!




Mwenzangu umeonaje hii Arusi?
Mimi nimeona kama hawana Furaha..sijui wamelazimishwa au Utiifu/Heshima...
Tunawatakia kila la kheri na Baraka.

Mengi sina karibu kwa Maoni Yako.

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.