Wataalam wa afya DMV (HCP Metro DC) wanatuleta huduma ya afya kwa wale wasiokuwa na bima ya afya. Huduma hii itatolewa kwa usawa bila kujali dini,rangi,umri,uraia au uchumi.
Kama una rafiki, ndugu au mzazi asiyekuwa na bima ya afya tunaomba mshiriki ili tuwe na jamii inayoshamiri na yenye afya njema. Zoezi hili litachukuwa hatua ya kuwaona wale watakaokuwa na hali pungufu ya afya njema mara moja kwa mwezi.
Tarehe: 04/12/2014 (Jumamosi)
Saa 3:00 asubuhi hadi mchana 7:00 (waweza kuja hata kwa saa moja)
MAHALA
3621 Campus Drive,
College Park, MD 20740
Leo hii wadau wetu tunaomba tujitolee kufanikisha huduma hii ya maangalizi ya afya ya bure kwa wadau wa DMV.
Unaweza kujitolea kwa namna mbalimbali
Tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe nesiwangublog@gmail.com ili tuweze kupata idadi na uhakika wa msaada wako.Unaweza kujitolea kwa namna mbalimbali
- Iwe ni kumsadia mtu usafiri,
- kuandikisha majina ya wanaokuja
- kubeba na kupanga meza kabla na baada ya maangalizi
- au kushiriki katika timu ya kitaalam
1 comment:
AFYA NDO MPANGO MZIMA...NI VEMA IZINGATIWE
Post a Comment