Wapendwa/Waungwana;Siku kama ya Leo Binti Yetu Mpendwa,Da'Tracey-Sarah,Alizaliwa.
Leo ametimiza miaka 13.Tunamshukuru sana MUNGU kwa Zawadi hii,Tunamtakia Masomo/Maisha Mema yenye Baraka,Amani,Upendo,Hekima.
Awe Baraka kwetu na Jamii pia.
Awe Kichwa na si Mkia.
MUNGU akumpe miaka mingi ,Akupe Maono/Njozi na Ukapate Kufanikisha Ndoto zako.
MUNGU azidi kumsimamia kila iitwapo Leo.
Mungu Ukawajaalie na wale wanaotafuta Watoto.
Shukrani kwa Wote Mnaoungana/Mlioungana/Mnaoendelea kuungana nasi Katika Malezi,MUNGU azidi kuwatendea kila lililo Jema.
Pia tunawatakia kheri na Baraka Watoto/Watu wote waliozaliwa siku kama ya leo.
Familia ya Isaac tunawapenda Wote na Asanteni kwa yoooote!!
"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.
1 comment:
Sijachelewa naanini....hongra dada Tracey kwa siku yako. Pongezi kwa wazazi pia
Post a Comment