Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 22 June 2014

Nawatakia JumaPili Njema na Yenye Amani;Burudani-Ambassador of Christ Choir Rwanda - Kaeni macho,Tuwe Na Upendo,Ng'ambo Ya Mto...!!!!!

Wapendwa Nawatakia JumaPili njema,Yenye,Amani,Upendo na Furaha..........
Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa;Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa;Achilieni, nanyi mtaachiliwa;Wapeni watu vitu,nanyi mtapewa;kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu.Kwa kuwa kipimo kile kile  mpimacho ndicho mtakachopimiwa............

Neno La Leo;Luka Mtakatifu:6:1-49

43.Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya,Wala mti mbaya uzaao matunda mazuri;44.Kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake;Maana,katika miiba hawachumi tini,wala katika michongoma hawachumi zabibu.45.Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, Na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu;Kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Suala juu Ya Siku Ya Sabato;1-5
Mtu mwenye mkono Uliopooza;6-11
Yesu anateuwa Mitume kumi na wawili;12-16
Yesu anafundisha na Kuwaponya watu;17-19
Heri Na Ole;20-26
Kuwapenda Maadui;27-36
Juu Ya Kuwahukumu Wengine;37-42

Mtu Hujulikana kwa Matunda Yake;43-45
Wajenzi wa NamnaMbili;46-49








Mhhhhmmmm;Tuache Maneno Yesu yu karibu tena yukaribu sana siyo mbaliiii,Hatujui siku wala saa Ndugu....Lakini dalili zinaonyeshaaa....
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Iwe njema kwenu Pia!

Rachel Siwa said...

Asante sana Kadal,ilikuwa njema kabisa.