1Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia. 2Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.
3Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa.4Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, 5mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.
Neno La Leo;Mwanzo1:1-31
26Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” 27 Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. 28Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”
Bible Society of TanzaniaYou have removed my shame,
You take as I am
You call me justified,
Now I am covered by Your grace
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.
No comments:
Post a Comment