MAMA MALKIA WA UPENDO 💎
💞MAMA MTUMWA WA MAPENZI💞 💎
🌾🍃Mwanadamu ulizaliwa katika hisia za kulia ukiwa kichanga mwenye uchafu Asili ya upendo ipo kwa mama ulipofumbua macho ulikutana na tabasamu la mama.
🌾🍃Mama alitabasamu wakati unalia mama alijifanya uchizi ili kukufurahisha ghafla ungetokea kuwaona mtoto anapocheza na mama yake ungelidhani wote ni watoto kwa mapenzi ya mama.
🌾🍃Mwanadamu tambua unaweza umizwa na wengi lakini upendo wa mama ukakufanya utulie na hakuna mapenzi ya kweli kwa mtu kama mapenzi ya mama.
🌾🍃Mama juu yako baya likikukuta mama hulia mama yupo tayari kudanganya ulimwengu kukukomboa katika matatizo yako.
🌾🍃Alificha chakula wakati ukicheza udogoni na uliporejea ukamkuta amelala lakini aliacha maagizo utakuta wapo wa kukupashia yote mapenzi.
🌾🍃Mama alipoamka mwanzo alikuulizia ameshakula? Ima umekula atafurahi ima hujala atapita majumba ya watu kukuulizia hata kama atatoka miguu peku yote mapenzi tu.
🌾🍃Ulipoumwa usiku halali atataabika kwa kukaa na wewe ukiwa mikononi mwake huku akilalila ukuta pembeni mwa kitanda huku akitarajia pakikucha shingo limuume kwa kukesha na wewe yote mapenzi hayo.
🌾🍃Mtu yoyote akikupenda watu watamshangaa kwanini anakupenda sana? Lakini mapenzi ya mama hayaulizwi kwanini anampenda yote ni nguvu za hisia za upendo toka kwa mama.
🌾🍃Umekuwa sasa huenda hayupo tena mama amekuacha katika dunia ya mihangaiko na wala tambua hakuna tena kiumbe kitachokupenda kama alivokuwa mama.
🌾🍃Na ukiwa umebarikiwa upendo ulio hai kwako namaanisha uhai wa mama basi huenda amechokaa na anatembea kama mtoto sasa rudisha upendo wako kwa kumfanya nae afurahi japo hutoweza kulipiza yote.
🌾🍃Mama utamkumbuka utapomkosa utatamani kuita mama na hata ukipata wa kuwaita upendo hautatoka moyoni.
🌾🍃Wakati ulipotoka alitabasamu basi na wewe hakikisha wakati anakukimbia duniani mfanye atabasamu hata kama atatokwa na machozi .
🌾🍃Mtumie ujumbe huu Mama na kama hunae tena muombe kwa MOLA upatapo ujumbe huu watumie wenzako huenda wakafufua hisia kwa Mama.
🌾🍃HUYU NDIO MAMA MALIKIA WA UPENDO.
🌴🐪KISIWA CHA IMANI🐪🌴
Nimetumiwa na Rafiki Nami nimeileta hapa tujifunze sote.
"Swahili Na Waswahili" Pamoja Saima.
2 comments:
Imenigusa mno na nimemkumbuka sana mama........
Pole da'Yasinta...
Post a Comment