Wapendwa;Natumaini Jumapili inaendelea vyema,Iwe yenye Imani,Tumaini,Uponyaji,Faraja, Shukrani na Utukufu tumrudishie MUNGU.... |
1 Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima enyi viumbe vya mbinguni,
semeni Mwenyezi-Mungu ni mtukufu na mwenye nguvu.
2Semeni jina la Mwenyezi-Mungu ni tukufu.
Mwabuduni katika mahali pake patakatifu.
|
Neno La Leo Zaburi 29;1-11
Sauti ya Mungu katika dhoruba
(Zaburi ya Daudi)
3Sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya maji;
Mungu mtukufu angurumisha radi,
sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya bahari!
4Sauti ya Mwenyezi-Mungu ina nguvu,
sauti ya Mwenyezi-Mungu imejaa fahari.
5Sauti ya Mwenyezi-Mungu huvunja mierezi;
Mwenyezi-Mungu avunja mierezi ya Lebanoni.
6Huirusha milima ya Lebanoni kama ndama,
milima ya Sirioni kama mwananyati.
7Sauti ya Mwenyezi-Mungu hutoa miali ya moto.
8Sauti ya Mwenyezi-Mungu hutetemesha jangwa,
Mwenyezi-Mungu hutetemesha jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya Mwenyezi-Mungu huitikisa mivule,
hukwanyua majani ya miti msituni,
na hekaluni mwake wote wasema:
“Utukufu kwa Mungu!”
10Mwenyezi-Mungu ameketi juu ya gharika;
Mwenyezi-Mungu ni mfalme atawalaye milele.
11Mwenyezi-Mungu na awape watu wake nguvu!
Mwenyezi-Mungu na awabariki watu wake kwa amani!
|
"Swahili Na Waswahili"Muwe na Wakati Mwema.
2 comments:
Kachiki Nadhani sijachelewa kukutakia nawe pia jpili njema pamoja na familia. N ahsante kwa neno
Asante sana Kdala wa mimi, Ilikuwa njema kabisa..
Salaam hapo nyumbani.
Post a Comment