Wapendwa Nimatumaini yangu Jumapili hii ilikuwa/Inaendelea Vyema Nawataki kila lililojema,Amani,Furaha,Baraka na Fanaka. Utukufu tumarudishie MUNGU. |
5 Mwenyezi-Mungu ni mwema;
fadhili zake zadumu milele,
na uaminifu wake katika vizazi vyote.
Neno La Leo;Zaburi 100
Wimbo wa sifa
(Zaburi ya shukrani)
1Mshangilieni Mwenyezi-Mungu, enyi nchi zote!
2Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha,
nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!
3Jueni kwamba Mwenyezi-Mungu ni Mungu.
Yeye ndiye aliyetuumba, nasi ni mali yake;
sisi ni watu wake, ni kondoo wa malisho yake.
4Pitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani,
ingieni katika nyua zake kwa sifa.
Mshukuruni na kulisifu jina lake.
5 Mwenyezi-Mungu ni mwema;
fadhili zake zadumu milele,
na uaminifu wake katika vizazi vyote.
Bible Society of Tanzania
Bible Society of Tanzania
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.
2 comments:
Ni matumaini yangu nawe na familia pia wote waliokuzunguka mmekuwa na jumapili njema sana. Binafsi iliishia mzigoni:-)
Asante Kakdala wa mimi, ilikuwa njema.
Post a Comment