Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 14 April 2016

MBUNGE WA CHAMA CHA WAZALENDO ACT-TANZANIA AKUTANA NA WATANZANIA NEW YORK CITY



Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini akisisitiza jambo mbele ya vijana wa Kitanzania waishio New York. Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana hao waliotaka kujua maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya bunge la jamhuri anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi kupitia upinzani, pia yeye kama mwana siasa alie upande wa upinzani nini mtazamo wake juu ya kasi ya rais wa wamu ya 5. Zitto ni mmoja ya vijana kwenye Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na ni Mbunge mwenye nguvu na uwezo wa kuwakirisha hoja zenye mashiko ndani ya bunge la jamhuri na kuitikisa serikali ya chama tawala. Mfano mmoja ni suala la Escrow yeye ndiyo alikuwa chanzo cha habari hiyo iliyotikisa serikali na kupelekea wananchi kukosa imani na mwenendo mzima wa serikali ya chama tawala. Na pia alisha wasilisha hoja ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa ubunge kwa miezi 4. Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University  New York na kuongea na wasomi wa huko na pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard University huko Boston. MA.  Picha na Vijimambo Blog New York
Zitto akipata ukodak baada ya kukutana na Watanzania New York City. Kwa taswira   zaidi nenda soma zaidi.

Zitto  akitafakari swali kabla kujibu,  Zitto aliulizwa kama yupo tayari kuungana na Ukawa na kama yupo tayari kungombea kiti cha urais kupitia chama chake ACT, majibu yalikuwa yupo tayari kuungana na ukawa lakini anaitaji kujua nini faida ya kuungana na kama kuungana ili kuing'oa CCM basi iwe na nguvu kweli kweli na ifanikiwe kwani asinge penda kuungana na nakubakia msindikizaji tu bila faida endelevu na kama yupo tayari kugombea kiti cha urais basi atafanya hivyo akiwa amesha jiandaa vilivyo ili akigombea apata ushindi wa kishimdo na kuing'oa CCM na siyo vinginevyo.

Hapa ni Patel akiuliza swali kwa Zitto,  Patel ni Mtanzania mwenye asili ya India ndiyo aliandaa mkutano huu kwa kushirikiana na Nasaan Chiume.

Shabani Mseba akiuliza swali kwa Zitto swali lake nini mipango ya maendeleo jimboni kwake.
Na jibu lake lilikuwa  mipango yake ni kuhakikisha  elimu  inakuwa na mwamko ndani ya mkoa wake. Kwani elimu imeshuka sana na ufaulu wa watoto umezidi kuwa chini.

No comments: