Mimi mzee, nakuandikia wewe Gayo, rafiki yangu, ninayekupenda kweli.
Uaminifu wa Gayo
2Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni. 3Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakashuhudia juu ya uaminifu wako kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli. 4Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusikia kwamba watoto wangu wanaishi katika ukweli.
Uaminifu wa Gayo
5Mpenzi wangu, wewe ni mwaminifu kila mara unapowahudumia ndugu, hata kama ni wageni. 6Ndugu hao wamelieleza kanisa hapa habari za upendo wako. Tafadhali uwasaidie waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu. 7Maana wanaanza safari yao katika utumishi wa Kristo bila kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini.8Basi, sisi tunapaswa kuwasaidia watu hawa, ili nasi tupate kushiriki katika kazi yao kwa ajili ya ukweli.
Diotrefe na Demetrio
9Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye hupenda kuwa kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza. 10Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuza nje ya kanisa.
11Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
12Kila mtu anamsifu Demetrio; naam, ukweli wenyewe unamsifu. Nasi pia tunatoa ushahidi wetu juu yake, nawe wajua kwamba tunachosema ni kweli.
Salamu za mwisho
13Ninayo bado mengi ya kukuambia, lakini sipendi kuyaandika kwa kalamu na wino. 14Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana.
15Nakutakia amani. Rafiki zako wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu wote kila mmoja binafsi.
Bible Society of Tanzania
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
4 comments:
Jumapili yangu ilikuwa ya amani na afya tele na natumaini hata ww na familia yako pia waliokuzunguka ilikuwa hivyo. Nimependa picha zako unazidi kuwa kamwali kadala wa mimi:-)
umependeza sana,ubarikiwe
Asante sana Kadala wa mimi nafuata nyayo zako.
Asante sana @happyhomemagazine
Post a Comment