Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 6 April 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Kutoka 6...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu kwa maana Fadhili zake ni za milele..
Asante Mungu Baba kwa kutuchagua sisi na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..si kwamba sisi ni wema sana,kwamba ni wenyenguvu/utashi,si kwamba sisi ni bora mno, si kwamba wengine ni wakosaji sana hapana Baba wa Mbinguni ni kwa Neema/Rehema yako tuu..

Tazama Jana imepita Baba Leo ni siku mpya Kesho ni siku nyingine Yahweh...!!Tunakuja mbelezako tukijinyenyekeza na Tunaomba ukabariki maisha yetu Baba..Maisha yetu yapo mikononi mwako Jehovah..!!Wewe unatujua kuliko tunavyojijua Baba wewe ni Mungu wetu,Muumba wetu,wewe ni Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Wewe Ndimi Mwenyezi-Mungu ujapokuwa nasi hakuna linaloshindikana,Wewe ni kila kitu hakuna kama wewe na hatokuwepo..Wewe ni Alfa na Omega..!!!
Tunaomba utubariki Tuingiapo/tutokapo,vilaji/vinywaji,vyombo vya usafiri,tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..!!
Ukabariki kazi zetu,Biashara,Masomo na ukaguse na kutakasa vyote tunavyo enda kutumia,Ukatutakase Miili yetu na Akili zetu Baba wa Mbinguni na Damu ya mwanao mpendwa Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..Aliteseka na kumwaga damu ili sisi tupate kupona..
Tunakwenda kinyume na Mwovu, Nguvu za Giza,Nguvu za Mizimu,Nguvu za mapepo,Nguvu za Mpinga Kristo Zishindwe katika Jina la Bwana wetu Yesu  Kristo wa Nazareti...

“Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake. Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.” Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake. Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji. “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!” Roho na Bibi arusi waseme, “Njoo!” Kila mtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Aliye na kiu na aje; anayependa, na achukue maji ya uhai bila malipo.
Tunakuja mbelezako Baba tukiomba na utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe..kwakujua/kutojua,kwakunena/kwakutenda na kwakuwaza..
Baba ukatupe Neema ya sisi kuweza kuwasamehe wote waliotukosea.

Mfalme wa Amani tunaomba ukawaponye na ukawaguse wenzetu walio wagonjwa,wasiojiweza,wafiwa ukawe mfariji wao,wenye shida/tabu,waliokatika vifungo mbalimbali baba ukawaponye kimwili na kiroho..wanaopitia Magumu/majaribu..Baba Yatima na wajane na walidhurumiwa haki zao zikapatikane..
Jehovah..Yahweh..!!Mfalme wa Amani..Tunayaweka haya yote mikononi mwako..Sifa na Utukufu ni wako,Tukishukuru na kuamini wewe ni Mungu wetu..Jana Leo na hata milele na ilele..

Amina..!!

Mimi Yohane nayaandikia makanisa saba yaliyoko Asia. Nawatakieni neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi, na kutoka kwa Yesu Kristo, shahidi mwaminifu, wa kwanza kufufuliwa kutoka kwa wafu, na ambaye ni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeye anatupenda, na kwa damu yake ametufungua kutoka vifungo vya dhambi zetu, akatufanya sisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikie Mungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uwe utukufu na nguvu, milele na milele! Amina. Tazama! Anakuja na mawingu! Kila mtu atamwona, na hata wale waliomtoboa. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina. “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Nguvu , aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
Mungu aendelee kuwabariki.


1Lakini Mwenyezi-Mungu akamjibu Mose, “Sasa utaona jinsi nitakavyomtenda Farao; maana kwa nguvu atalazimika kuwaacha watu wangu watoke. Naam, kwa nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”

Mungu anamwita Mose

2 Taz Mwa 17:1; 28:3; 35:11; Kut 3:13-15 Mungu akamwambia Mose, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu. 3Nilimtokea Abrahamu, Isaka na Yakobo nikijulikana kama Mungu Mwenye Nguvu,6:3 Mungu mwenye nguvu: Kiebrania: El Shadai. ingawa kwa jina langu, Mwenyezi-Mungu, sikuwajulisha. 4Tena nilifanya agano nao kwamba nitawapa nchi ya Kanaani ambako waliishi kama wageni. 5Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha Waisraeli ambao wamelazimishwa kufanya kazi za kitumwa na Wamisri, nikalikumbuka agano langu. 6Kwa hiyo, waambie Waisraeli hivi, ‘Mimi ni Mwenyezi-Mungu! Mimi nitawatoa katika nira mlizowekewa na Wamisri. Nitawaokoeni utumwani mwenu. Nitaunyosha mkono wangu wenye nguvu na kuwaadhibu vikali Wamisri na kuwakomboa nyinyi. 7Nitawafanyeni kuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. Nyinyi mtatambua kuwa mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa katika nira za Wamisri. 8Nami nitawapeleka katika nchi ile niliyoapa kumpa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitawapeni nchi hiyo iwe yenu. Mimi ni Mwenyezi-Mungu.’” 9Mose akawaeleza Waisraeli maneno hayo. Lakini wao hawakumsikiliza kwa sababu walikuwa wamekufa moyo kutokana na utumwa mkali.
10Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 11“Nenda kwa Farao, mfalme wa Misri, umwambie awaache Waisraeli waondoke nchini mwake.” 12Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Tazama, Waisraeli hawanisikilizi mimi, sembuse Farao! Tena mimi ni mtu asiye na ufasaha wa kuongea!” 13Lakini Mwenyezi-Mungu akaongea na Mose na Aroni, akawaagiza waende kwa Farao, mfalme wa Misri, na kuwatoa Waisraeli nchini Misri.

Ukoo wa Mose na Aroni

14Hii ndiyo orodha ya wakuu wa jamaa za Waisraeli, Wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli: Henoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hao walikuwa mababu wa jamaa za Reubeni. 15Wana wa Simeoni walikuwa: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli; huyu wa mwisho alikuwa mtoto wa mwanamke wa Kikanaani. Hao walikuwa mababu wa jamaa za Simeoni. 16Taz Hes 3:17-20; 26:57-58; 1Nya 6:16-19 Sasa yafuata majina ya wana wa Lawi na wazawa wao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137. 17Wana wa Gershoni walikuwa: Libni na Shimei; jamaa zao zilitajwa kwa majina yao. 18Wana wa Kohathi walikuwa: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133. 19Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Hao ndio mababu wa jamaa za Walawi.
20Amramu alimwoa Yokebedi, shangazi yake, naye akamzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137. 21Na watoto wa kiume wa Ishari walikuwa: Kora, Nefegi na Zikri. 22Watoto wa kiume wa Uzieli walikuwa: Mishaeli, Elsafani na Sithri.
23Aroni alimwoa Elisheba, binti yake Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 24Nao watoto wa kiume wa Kora walikuwa: Asiri, Elkana na Abiasafu, ambao walikuwa mababu wa jamaa za Kora. 25Eleazari, mwana wa Aroni, alimwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio waliokuwa wakuu wa jamaa za Lawi.
26Aroni na Mose ndio walioambiwa na Mwenyezi-Mungu, “Watoeni watu wa Israeli kutoka nchi ya Misri, vikundi kwa vikundi.” 27Ndio haohao Mose na Aroni walioongea na Farao, mfalme wa Misri, juu ya kuwatoa Waisraeli nchini Misri.

Mungu amwamuru Mose na Aroni

28Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoongea na Mose nchini Misri, 29alimwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. Mwambie Farao, mfalme wa Misri, maneno yote ninayokuambia.” 30Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Mimi sina ufasaha wa kuongea; Farao atanisikilizaje?”

Kutoka6;1-30

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: