Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Asante Mungu wetu Baba yetu,Asante kwa wema na fadhili zako kwetu.. Asante kwa ulinzi wako usiku na siku zote umekuwa nasi Jehovah.. Asante kwakutuchagua tena na kutupa Kibali cha kuendelea kuiona leo hii.. Si kwa uwezo wetu wala nguvu zetu ni kwa Neema/Rehema yako tuu Mungu wetu sisi kuwepo leo hii na kuweza kufanya yote haya tufanyayo..
Tazama Jana imepita Baba wa Mbinguni Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine Jehovah.. Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Yahweh..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wote waliotukosea..
Roho mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi.. Utuepushe na majaribu ya yule mwovu na kazi zake..Utuokoe na kutufunika na Damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti.. Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..
Tukaanze nawe Bwana wetu katika wiki hii..yote tunayoenda kufanya/kutenda yakaendane na matakwa yako Jehovah..
ukaonekane kwenye maisha yetu Yahweh..!ukatupe hekima,Busara katika kuamua na kutenda,tukapate kutambua/kujitambua.. Tukaelewe na kulijua Neno lako,Tukafuate na tukatii sheria zako na Amri zako
Tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Kila kuhani mkuu ambaye huchaguliwa miongoni mwa watu hupewa jukumu la kushughulikia mambo ya Mungu kwa niaba ya watu, kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya dhambi. Maadamu yeye mwenyewe ni dhaifu, anaweza kuwatendea kwa huruma wale wasiojua kitu na wanaofanya makosa. Kwa sababu hiyo anapaswa kutoa tambiko si tu kwa ajili ya watu, bali pia kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe. Hakuna mtu awezaye kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kama alivyokuwa Aroni. Hali kadhalika naye Kristo; yeye hakujitwalia mwenyewe heshima ya kuwa kuhani mkuu, bali Mungu alimteua na kumwambia: “Wewe ni Mwanangu; mimi leo nimekuwa baba yako.” Alisema pia mahali pengine: “Wewe ni kuhani milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.” Yesu alipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kilio kikuu na machozi, alisali na kumwomba Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kifoni; naye alisikilizwa kwa sababu ya kumcha Mungu. Lakini, ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, alijifunza kutii kwa njia ya mateso. Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii, naye Mungu akamteua kuwa kuhani mkuu kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.
Ukatuongoze ee Mungu wetu na ukatubariki na kubariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi utupe neema ya kuwabariki wenyekuhitaji..
Neno lako likawe Mwanga kwenye maisha yetu likawe faida na likatufae sisi na wengine pia.. Wale walio asi wakapate kurudi kundini na kuwa pamoja katika kuamini na kujifunza zaidi..
Tunayo mengi ya kusema juu ya jambo hili, lakini ni vigumu kuwaelezeni, kwa sababu nyinyi si wepesi wa kuelewa. Kwa wakati huu nyinyi mngalipaswa kuwa waalimu tayari, lakini mnahitaji bado mtu wa kuwafundisheni mafundisho ya mwanzo juu ya neno la Mungu. Mnahitaji maziwa badala ya chakula kigumu. Kila anayepaswa kunywa maziwa ni mtoto bado, hajui uadilifu ni nini. Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu waliokomaa, waliofunzwa kwa vitendo kubainisha mema na mabaya.
.Baba wa Mbinguni ukaonekane kwenye Maisha yetu na tusipungukiwe na mahitaji yetu..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako,Tukiamini wewe ni Mungu wetu hatuna Mungu mwingine.. Yote tuliyoyanena na kutonena Baba unayajua na unatujua kuliko tunavyojijua.. Mungu wetu ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu.. Kwakua Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Mungu aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake.. Niwashukuru sana kwakunisoma/kupita hapa.. Nawapenda. |
No comments:
Post a Comment