Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 23 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..21...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake..
Asante Baba wa Mbinguni kwa ulinzi wako wakati wote...
Asante kwakutuamsha tena wenye afya na kuweza kuendelea na majukumu yetu..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..
Sifa na utukufu una wewe Mungu wetu,Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo....
Muweza wa yote,Alfa na Omega,Yahweh..!Jehovah Baba wa upendo,Baba wa Amani,Mponyaji,Mfariji,Hakuna kama wewe Mungu wetu...


Tunakuja mbele zako Mungu wetu tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..

Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Utuepushe na majaribu ya yule mwovu na kazi zake zote..
Utukokoe na ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..

yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..




Enyi watumishi wa nyumbani, watiini wakuu wenu kwa heshima yote, wawe wema na wapole au wenye kuchukiza. Maana kama mnavumilia maumivu ya mateso msiyostahili kwa sababu mwajua kwamba Mungu anataka hivyo, basi Mungu atawafadhili. Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo. Hayo ndiyo mliyoitiwa; maana Kristo mwenyewe aliteseka kwa ajili yenu, akawaachieni mfano, ili mfuate mwenendo wake. Yeye hakutenda dhambi, wala neno la udanganyifu halikusikika mdomoni mwake. Alipotukanwa yeye hakujibu kwa tukano; alipoteseka yeye hakutoa vitisho, bali aliyaweka matumaini yake kwa Mungu, hakimu mwenye haki. Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake juu ya msalaba, tupate kufa kuhusu dhambi, na kuishi kwa ajili ya uadilifu. Kwa majeraha yake, nyinyi mmeponywa. Nyinyi mlikuwa kama kondoo waliokuwa wamepotea; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote tupate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..


Tazama wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu ukawaguse  kwa mkono wako wenye nguvu na wakapate kupona kimwili na kiroho pia..Mungu wetu ukaonekane na kuwafuta machozi wanaokulilia na ukawajibu wanaokuomba na ukawaongoze na kuwapa macho ya kuona na masikio ya kusikia waliopotea warudi zizini kwako....
Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.


Mungu wetu tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..

Mungu wetu utuepushe na tamaa mbaya,ukatili,kuhukumu wengine na yote yasiyokupendeza wewe...
Ukatupe neema ya Upendo,Utuwema,Hekima,Busara,Heshima kwa watu wote,Utii,Unyenyekevu,tuelekezane/kuonyana kwa upendo na Upole kiasi....
Tukawe Barua  njema popote tupitapo na tusomeke sawasawa na mapenzi yako...

Mungu wetu ukatuweke huru na tusitumie vibaya uhuru na kwenda kinyume nawe....


Wapenzi wangu, nawasihi nyinyi kama wageni na wakimbizi hapa duniani! Achaneni na tamaa za mwili ambazo hupingana na roho. Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ili hata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze kutambua matendo yenu mema na hivyo wamtukuze Mungu siku ya kuja kwake. Basi, jiwekeni chini ya mamlaka yote ya kibinadamu, kwa ajili ya Bwana: Utii kwa mfalme aliye mtawala mkuu, utii kwa wakuu wa mikoa ambao wameteuliwa naye kuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendao mema. Maana Mungu anataka muweze kuyakomesha maneno ya kijinga ya watu wasio na akili kwa matendo mema mnayofanya. Ishini kama watu huru; lakini msiutumie uhuru wenu kuuficha ubaya, bali ishini kama watumishi wa Mungu. Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu zenu waamini, mcheni Mungu, mheshimuni mfalme.

Mungu wetu ukabariki Nyumba/familia zetu,Ukawalinde watoto wetu katika makuzi/ujana wao na wakawe na hofu ya Mungu..

Sifa na utukufu tunakurudishia Mungu wetu..
Tunashukuru na kukuabudu daima..
Yote tunayaweka mikononi mwako Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Wapendwa ninawashukuru sana kwa muda wenu..

Asanteni sana Mungu aendelee kuwabariki..
sina neno zuri zaidi la kusema
Mungu akaonekane kwenye maisha yenu..
Nawapenda.

Maisha ya ukuhani
1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Waambie makuhani, wana wa Aroni, kwamba pasiwe na mtu yeyote miongoni mwao atakayejitia najisi kwa kugusa maiti ya watu wa jamaa yake, 2isipokuwa kama ni maiti ya ndugu yake wa karibu, yaani mama yake, baba yake, mwanawe, binti yake, ndugu yake 3au dada yake ambaye (aliye wa jamaa yake ya karibu), naye hajaolewa bado. 4Yeye, akiwa mwenye madaraka katika jamaa yake, asijitie unajisi.#21:4 mstari huu si dhahiri katika Kiebrania. 5#Taz Lawi 19:27-28; Kumb 14:1 Wazawa wa Aroni kamwe wasijinyoe upara kuomboleza wala wasikate pembe za ndevu zao wala kujichanja chale mwilini. 6Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao wala wasilikufuru jina la Mungu wao. Maana wao ndio wanaotolea zile sadaka anazopewa Mwenyezi-Mungu kwa moto yaani chakula cha Mungu. Basi, ni lazima wawe watakatifu. 7Kwa kuwa kuhani amewekwa wakfu kwa Mungu wake, kamwe asioe kahaba, wala mwanamke asiye bikira wala aliyepewa talaka. 8Utamtambua kuhani kuwa aliyewekwa wakfu, maana yeye ndiye anayetoa sadaka ya mkate wa Mungu wako; utamtambua kuwa mtakatifu, maana mimi Mwenyezi-Mungu ninayekuweka wewe wakfu, ni mtakatifu. 9Binti wa kuhani yeyote akijitia unajisi kwa kufanya ukahaba, atateketezwa kwa moto kwani anamtia baba yake unajisi.
10“Kuhani mkuu yeyote, kwa kuwa yeye ni mkuu kati ya ndugu zake, naye amemiminiwa mafuta ya kupaka kichwani pake, na kuwekwa wakfu ili ayavae mavazi matakatifu, asiache nywele zake kuwa ovyo wala asirarue mavazi yake kuomboleza. 11Asikaribie maiti wala kujitia unajisi kwa maiti hata kama ni ya baba yake au ya mama yake. 12Kwa kuwa amewekwa wakfu kwa kupakwa mafuta ya Mungu wake kichwani, basi asiondoke mahali patakatifu wala asipatie unajisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. 13Kuhani mkuu aweza tu kumwoa msichana ambaye ni bikira. 14Haruhusiwi kuoa mwanamke mjane, mwanamke asiye bikira, wala kahaba. Ni lazima aoe bikira kutoka watu wake mwenyewe 15asije akawatia unajisi watoto wake mwenyewe. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyemweka wakfu.”
16Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 17“Mwambie Aroni hivi: Mzawa wako yeyote katika vizazi vyote vijavyo ambaye ana dosari mwilini, haruhusiwi kukaribia na kunitolea mimi Mungu wake sadaka ya mkate. 18Mtu yeyote mwenye dosari sikaribie kunitolea sadaka: Awe kipofu, aliyelemaa, aliyeharibika uso, mwenye kiungo kirefu kuliko kawaida, 19mwenye mguu au mkono ulioumia, 20mwenye kibyongo, mtu mfupi kuliko kawaida, mwenye macho mabovu au ugonjwa wa ngozi, mwenye upele au towashi. 21Mzawa yeyote wa kuhani Aroni mwenye kilema asikaribie kunitolea sadaka za kuteketezwa kwa moto; kwa vile ana kilema, basi, asikaribie kunitolea mimi Mungu mkate wangu. 22Mtu huyo anaweza kula mkate wa Mungu wake, vitu vitakatifu na vile vitakatifu kabisa. 23Lakini asilikaribie lile pazia wala ile madhabahu kwani ana dosari, asije akapatia unajisi mahali patakatifu; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu ndiye ninayewaweka wakfu.”
24Mose akamweleza Aroni na wanawe na Waisraeli wote mambo hayo yote.

Mambo Ya Walawi21;1-24


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: